Profesa
Innocent Ngalinda Mtaalam Mshauri wa takwimu akitoa mada katika warsha
ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi iliyoandaliwa na
Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood
Tanzania (WRATZ)ambapo mambo mbalimbali yanajadiliwa na wadau kutoka
taasisi mbalimbali hapa nchini ili kutatua changamoto zinazokabili
huduma ya Mama na mtoto, Warsha hiyo inafanyika kwenye hoteli ya Regency
Park Mikocheni jijini Dar es salaam
Bi.
Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for
Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo wakati alipokuwa
akitoa mada katika Warsha hiyo iliyojadili mambo mbalimbali yanayohusu
kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na salama kwa mama na
mtoto nchini.
Kutoka
kushoto ni Tausi Sued kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas
International ya Marekani, Angelina Ballat kutoka Taasisi ya Childbirth
Survivas International, Julieth MawallaKutoka Halmashauri ya Wilaya
Ubungo na Sara Luaimay kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni
wakifuatilia mjadala huo.
Anna
Sawaki Ofisa Mawasiliano na Habari Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon
Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo katika
warsha hiyo.
Dr
Brenda Squetra D' Mello Daktari Mshauri wa Afya ya Mama na Mtoto
Hospitali ya CCBRT akichangia mada katika warsha hiyo iliyofanyika
kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo.
Bi.
Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for
Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifuatilia mada pamoja na washiriki
wengine katika warsha hiyo.
Bi.
Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for
Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akitolea ufafanuzi kwa waandishi wa
habari mambo mbalimbali yaliyojadiliwa katika warsha hiyo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KATIKA
kuhakikisha Vifo vinavyotokana na uzazi kwa kina Mama vinapungua,Jamii
imehimizwa kumpeleka mzazi kwenda kwenye vituo vya Afya ambavyo vina
wataalamu ,kwani hatua hiyo ndio njia ya kusaidia kuondokana vifo hivyo.
Hayo
yamebainishwa na Mratibu Taifa wa Muungano wa UtepeMweupe na Uzazi
Salama, Rose Mlay wakati wa mkutano wa wadau wakati wa Mkutano wa Wadau
wa Afya na Mama na Mtoto uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema
kuwa kupoteza mtoto na mama ni ajali ambayo inatokana na kukosekana kwa
huduma sahihi wakati wa kujifungua.
Amesema
kuwa mkutano wadau ni pamoja na kujadili takwimu za Afya ya Mama na
Mtoto pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi.
Mlay
amesema kwa sasa vifo vya wakina Mama vimeongezeka kutoka kwa vifo 24
vya wakinamama kwa siku hadi kufikia vifo 30 kwa siku huku akisema
ongezeko hilo limechangiwa na wakina Mama kujifungulia sehemu zisizo
salama,
"Ripoti
inaonyesha vifo vinaongezeka kutokana na kukosekana kwa vituo vya afya
vyenye pamoja na wataamu kama nyumbani na kwenye vituo visivyo na
watalaamu,unakuta sehemu hakuna vifaa vya kumsaidia Mama ili aweze
kujifungua salama,na hii inasababisha vifo hivi kuongekezeka"
".Amesema
jamii kama ingekuwa inampeleka Mzazi kwenye vituo vya afya vyenye ubora
basi vifo hivi vingepungua ikiwezekana kumalizika kabisa"Amesema Mlay.
Mlay
amesema Takwimu za hapo awali zilionyesha kuwa takribaniwanawake 8000
hufaliki kila mwaka kwa sababu ya Matatizo yanayotokana na Mimba na
Uzazi lakini Takwimu hizo zimeongekeza hadi kufikia zaidia ya elfu 10
kwa mwaka .
Kwa
upande wao Wadau mbalimbali waliokuwepo kwenye Mkutano huo ,wameitaka
serikali kuhakikisha inaongeza bajeti kwenye sekta ya Afya ambayo
itavisaidia kwenye vituo vya Afya kuwepo kwa wakunga wenye welevu na
ujuzi ambao watasaidia kupunguza vifo hivo.
No comments:
Post a Comment