Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye shati jeupe ) akiongozana na
viongozi mbalimbali kukagua mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga
jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na
mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.
Na Tiganya Vincent- RS-Tabora
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imeawaagiza Maafisa Ugani kuanza mapema maandalizi ya
kilimo cha pamba kwa wakulima kutoka wilaya tano mkoani hapo
zilichaguliwa kulima zao ili waweze kuzalisha pamba nyingi na nzuri kwa
ajili viwanda mbalimbali hapa nchini.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani
Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya Kiwanda cha Pamba cha
Manonga wilayani Igunga ambacho kimekuwa hakifanyi kazi kwa miaka zaidi
ya 20 kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa pamba ya kutosha.
Alisema
kuwa watendaji wote wanaohusika na usimamizi wa zao la pamba ni vema
wakahakikisha kuwa wakulima wanapanda mbegu zinazotakiwa na kwa nafasi
inayoshauri kitaalamu na kutimia mbolea na dawa za kuua wadudu
zinazotakiwa.
Mwanri
alisema kuwa Tabora imepata mbegu bora tani 500 ambazo zitasaidia
kusambazwa katika Wilaya ambazo zimechaguliwa kulima zao la Pamba za
Kaliua, Urambo, Nzega, Igunga na Uyui.
Alisisitiza pamba itakayolimwa na kuvuna itauzwa kupitia Vyama vya Ushirika na sio vinginevyo ili kuepuka mkulima kunyonywa.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa alipiga marufuku matumizi ya mbegu ambazo
hazikuidhinishwa na Bodi ya Pamba na kuingiza mkoani hapa dawa ambazo
zimepitwa na wakati.
Alisema
kuwa atakayebainika atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na
kufikishwa katika vyombo vya sheria ili apate adhabu inayostahili.
Naye
Meneja wa Kanda wa Bodi ya Pamba Jones Bwahama alisema kuwa wilaya ya
Igunga mkoani Tabora imechaguliwa kuwa kitalu cha taifa cha uzalishaji
wa mbegu za zao hilo , hivyo ni vema wataalamu wakawasaidia wakulima
kuzingatia maelekezo ya kitaalamu wakati wote wa ulimaji na uvunaji ili
kuwezasha maeneo megine yaje kuchukua mbegu.
Alisema
kuwa uzembe wowote utakaofanyika na kusababisha uharibifu wa mbegu hiyo
utakuwa umekwamisha juhudi za Serikali za kufufua zao la pamba hapa
nchini.
Bwahama
alitoa wito kwa Kampuni za ununuzi wa pamba katika Wilaya ya Igunga
katika kupata mbegu bora, dawa bora kwa ajili ya kuwakopesha wakulima
ili waweze kuzalisha pamba nzuri na bora.
Kwa
upande wa Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alisema kuwa msimu ujao
wanatarajia kuzalisha pamba nyingi zaidi ya mwaka uliopita kwa sababu
ulikuwa mwanzo hivi wameongeza nguvu katika kuwatembelea wakulima na
kuwahamasisha juu ya kilimo bora cha zao hilo.
Alisema
kuwa wanataka kuongeza kutoka kilo 10,700,000 ili ziwe zaidi ya hapo
kwa ajili ya kuongeza kipato cha wakazi wa Igunga na Halmashauri yao.
Mwaipopo
alisema kuwa ili kufanikisha zoezi hilo viongozi wilayani humo
wamejipanga kupita kwa wakulima ili kuwaelimisha ikiwa ni pamoja na
kuwaeleza juu ya matumizi ya mbegu bora na dawa za kuua wadudu kwa ajili
ya kuongeza uzalishaji.
Naye
Mkaguzi wa Pamba Wilaya ya Igunga George Kihimbi alisema kuwa
wanatarajia kuanza mikutano ya kuelimisha wakulima ili waweze kufuata
masharti ulimaji wa zao hilo kwa ajili ya kuwasidia kupata mazao mengi
na yenye tija.
Alisema
kuwa tayari wameshatayarisha vifaa mbalimbali kufundishia ikiwemo kamba
kwa ajili ya upimaji mashamba ambapo watawaelimisha wakulima juu ya
ulipandaji wa miche 22,000 katika heka moja ili wapate kilo 600.
Hivi
karibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim
Majaliwa alikutana Wakuu wa Mikoa inayolima pamba nchini na kuwaagiza
kuhakikisha wanasimamia zao hilo ili lirudi katika hali yake ya siku za
nyuma ambalo liliitwa dhahabu nyeupe.
No comments:
Post a Comment