Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Rans Nassor Salim Khamis inayojenga vituo 15 vya afya vya
Mradi wa Orio alipotembelea kituo cha Kiboje wa pili (kulia) Meneja
Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitembelea ujenzi wa kituo kipya cha afya
Kiboje akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa (kushoto)
meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor.
Meneja
wa Ujenzi wa Kampuni ya Rans Ali Nassor akimpa maelezo Waziri wa Afya
juu ya ukarabati wa kituo cha afya cha Uroa alipofanya ziara ya
kutembelea vituo vya Mradi wa Orio.
Muonekano
wa kituo kipya cha afya cha Kijini Matemwe kinachojengwa kwa
ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Uholanzi
kupitia Mradi wa Orio.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Kijini Matemwe baadaya kuangalia maendelea ya ujenzi wa kituo kipya cha
afya cha kijiji hicho.
Mafundi
wa Kampuni ya Rans wakiendelea na ujenzi katika kituo kipya cha afya
cha Chaani kubwa Wilaya Kaskazini A.Picha na Makame Mshenga.
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendeleza dhamira yake ya kuleta mabadiliko
makubwa katika sekta ya afya kwa kuimaisha huduma za afya na kujenga
vituo vyenye hadhi vijijini.Dhamira hiyo inaendelea kutekelezwa kwa
pamoja na wafadhili wa maendeleo wanaunga mkono juhudi zinazochukuliwa
na Serikali katika kufikiaq malengo hayo.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo alipotembelea vituo vitatu
vipya vya afya vya Kiboje, Kijini Matemwe na Chaani kubwa na kituo cha
Uroa kinachofanyiwa ukarabati mkubwa.Amesema serikali ya Uholanzi kwa
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia mradi wa Orio
hivi sasa unaendelea na ujenzi wa vituo 15 vya afya nane vikiwa
vinajengwa Unguja.
Waziri
Mahmoud aliwaeleza wananachi wa sehemu hizo kuwa lengo la kujengwa
vituo hivyo nikuwasogezea huduma za afya karibu na sehemu wanazoishi na
kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali kuu za
mijin.Amewahakikishia wananchi kuwa vituo vinavyojengwa kupitia mradi wa
Urio vitakapomalizika vitakuwa na vifaa vya kisasa na vitatoa huduma
zote muhimu zikiwemo wodi za kujifungulia.
Aliongeza
kuwa Wizaara ya Afya inajiandaa kuhakikisha kuwa vituo vyote
vinavyojengwa vinakuwa na wafanyakazi wa fani zote muhiumu ili
kuwapunguzia shida.“Wananchi wa Kijini kituo chenu ambacho ni cha daraja
la pili kitakapomalizika kitatoa huduma zote muhimu na wagonjwa
watatoka mjini kuja kutafuta matibabu hapa,”Waziri aliwahakikishia.
Amewataka
wananchi wanaoishi karibu na vituo hivyo vitakapomalizika kuvitumia
kikamilifu ili kuwapunguzi gharama za kufuata huduma ya matibabu
Hospitali kuu ya Mnazimmoja.Hata hivyo amewaomba akinababa wa Kijini na
Chaani kushirikiana na wake zao katika kupanga uzazi kwani kiwango cha
kuzaa katika maeneo hayo kimekuwa kikubwa.
“Kama
hamtashirikiana baba na mama katika kupanga uzazi itafika wakati kitanda
kimoja kitakuwa na wazazi wanne jambo ambalo halipendezi,”
aliwatanabahisha Waziri wa Afya .Aliwataka vijana kushirikiana na wazee
katika kuvilinda na kuvitunza vituo hivyo vya afya wakijua kuwa ni mali
yao na vinahitaji kukaa muda mrefu kutoa huduma.
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Mohamed aliwaeleza wananchi kuwa
vituo vyote vya afya vya daraja la pili vitakuwa na nyumba ya daktari na
vitatoa huduma za uzazi kwa saa 24.Dkt. Fadhil alisema huduma nyengine
za kawaida zitatolewa katika muda wa kawaida wa kazi na akitokea mgonjwa
wa dharura baada ya saa za kazi atahudumiwa.
Meneja
wa ujenzi wa vituo hivyo Ali Nassor Al Miskry wa Kampuni ya Rans
amemuhakikishia Waziri wa Afya kuwa ujenzi wa vituo hivyo utakamilika
mwezi Disemba na Januari mwakani vitaanza kutumika.
Alisema
vifaa vitakavyotumika katika vimeshapakiwa katika meli na vinatarajiwa
kuwasili mwisho wa mwezi wa kumi na kazi ya kuvifunga zitafanyika mara
baada ya ujenzi kukamilika.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO
No comments:
Post a Comment