SERIKALI
ya Tanzania, imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF)
kwa kuwezesha watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi
wanayoidhamini au kuitafutia fedha. Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa
ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya
rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa
kupeleka madaraka kwa umma na shughuli za maendeleo ya kiuchumi .
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu
Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa kongamano
la siku 2 la Wadau wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la Kalemawe
lililoko wilaya ya Same mwishoni mwa wiki.
“Tunafurahishwa
kwa namna ya pekee na UNCDF kwa jitihada zake zinazoendeshwa kupitia
katika Mpango wa Ufadhili Miradi ya kiuchumi (LFI),” alisema Iyombe na
kuongeza: “Tunapokutana hapa tunapewa fursa na kufunuliwa uzoefu wa
ushiriki wa UNCDF katika miradi mbalimbali, safari hii tukishuhudia
hatua yake ya kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika Mkoa
wa Kilimanjaro.” Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo
kuhusu mradi wa ufugaji samaki katika shamba hilo kwa viongozi
mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya
ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya
Bagamoyo. Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mh. Naghenjwa
Kaboyoka na Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki
pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (wa pili kulia).
Pamoja
na kushukuru kwa hatua mbalimbali zilizofikiwa na taasisi hiyo katika
kusaidia watanzania, aliwataka wakazi wa Same kuhakikisha kwamba mradi
huo ulioundiwa kampuni ili kwenda kibiashara unafanikiwa na kuwa mfano
kwa wengine. Halmashauri ya wilaya ya Same, na jamii inayozunguka bwawa
la Kalemawe wanashirikiana na UNCDF kuboresha miundo mbinu ya bwawa hilo
na kuwezesha uwapo wa uwekezaji kwa kuanzisha kampuni.
Kampuni
hiyo iliyosajiliwa ya Kalemawe Dam Investment Limited katika mpango
maalum (SPV) inamilikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya
wilaya ya Same, halmashauri ya vijiji sita, wakala wa serikali, watu
binafsi pamoja na makundi ya kijamii. Kuwapo kwa kampuni hiyo ni juhudi
zinazofanywa za kuwezesha uhusiano mahsusi wa kibiashara unaohusisha
ubia wa Serikali, Binafsi na jamii (PPCP) kwa kutoa umiliki linganifu
mpaka katika ngazi za chini za mamlaka za kijiji, ambazo kimsingi ndizo
wamiliki wa maliasili muhimu ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya
Vijiji ya Mwaka 1999. Viongozi
mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) wakiwa kwenye ziara fupi ya mafunzo
kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba la ufugaji samaki la
Ruvu lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Mradi
huo wa Ufugaji wa Samaki Kibiashara wa Bwawa la Kalemawe ni zao la
ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, Kata za Ndungu na
Kalemawe, asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo walioazimia
kukarabati na kufufua bwawa hilo na mfumo wake wa kilimo cha
umwagiliaji. UNCDF kwa kushirikiana na wabia wake waitwao Mikono Tayari
(ambao ni kundi linaloundwa na washirika kutoka Tanzania na Norway) ni
wataalamu katika mradi hu wa ufugaji samaki kwa pamoja na SPV ya Same na
washirika wake.
Katika
kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Staki amesema wilaya
yake ipo tayari kutekeleza mradi huo ambao una manufaa makubwa si tu kwa
watu wa Kalemawe na vijiji vinavyozunguka bali pia na halmashauri ya
wilaya ya Same. Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo
kuhusu vyakula vinavyotumika kulisha samaki wanaofugwa kwenye shamba
hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi
ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo
lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Akishiriki
katika mjadala aliwataka wanakalemawe kutambua umuhimu wa mradi huo na
kwamba hicho ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa watu binafsi na jamii
kwa ujumla. Mradi huo ambao ni sehemu ya programu kubwa ya kubadili watu
wenye makazi kuzunguka bwawa hilo umelenga katika siku za usoni
kuzalisha samaki na vifaranga vyake.
Ili
kuwa na uelewa mkubwa wa kufanya biashara hiyo ya samaki, madiwani na
wenyeviti wa serikali za mitaa za vijiji vinavyotengeneza kampuni hiyo
ya Kalemawe walitembelea shamba la samaki Ruvu ambapo waliona shughuli
mbalimbali zinazoendelea katika shamba hilo ili iwe mfano kwao Pamoja na
kuuza samaki shamba hilo ambalo lipo kilomita 20 kutoka Bagamoyo na
kilomita 13 hivi kutoka Mlandizi linafuga samaki aina ya sato na
hutotolesha vifaranga laki moja kila wiki kwa kulingana na oda
zilizopo. Ziara
ya mafunzo ikiendelea katika shamba la kufuga samaki la Ruvu lililopo
wilayani Bagamoyo. Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (wa pili
kushoto) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (katikati) pamoja na ujumbe
ulioambatana nao kwenye mafunzo hayo ukitazama jambo katika shamba hilo.
Mmoja
wa viongozi katika mradi huo Khumbo Kanthenga alisema kwamba mradi huo
ambao bado unapanuliwa kufikia mabwawa sitini kwa sasa umelenga kutoa
vifaranga kwa mujibu wa oda na pia kuuza samaki ambao wapo tayari
kuingia sokoni samaki hao wanafikia gramu 350 na kuendelea. Naye Mbunge
wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka ambaye alikuwapo katika kongamano
hilo alielezea haja ya wananchi wengi kutambua mipaka yao na kuhakikisha
kwamba dhamira safi iliyopo ya kufufua bwawa hilo na kubadilisha maisha
ya wananchi inafikiwa.
Wakifunga
Kongamano hilo UNCDF ili shukuru ushirikiano mkubwa wa karibu ambao
umeonyeshwa na washiriki wa warsha hii ya wadau kuanzia serikali kuu,
mkoa, willaya na viongozi wa vijiji sita vinavyohusika na utekelezaji wa
mradi na pia iliahidi kua mashirika mengine ya umoja wa mataifa
watashirikishwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huu na miradi
mingine mbalimbali katika eneo hili la bwawa la samaki. Eneo
ambalo linaandaliwa kwa ajili ya bwawa la kufugia samaki katika shamba
la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamayo. Wafanyakazi
wa shamba la kufugia samaki la Ruvu wakitega nyavu kwa ajili ya
kuonyesha samaki katika moja ya mabwawa kwenye shamba hilo wakati wa
ziara hiyo fupi ya mafunzo. Mmoja wa wafanyakazi wa shamba hilo akiwa ameshikilia samaki aina Sato wanaofugwa kwenye shamba hilo. Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (tisheti nyekundu) akitoa
maelezo katika chumba maalum cha kutotolea vifaranga vya samaki kwa
viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliokuwa kwenye ziara fupi ya
kupata elimu juu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo
lililopo wilaya ya Bagamoyo. Mshauri
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede akitazama mabwawa ya samaki
katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo. Mkurugenzi
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Daudi Makobole (wa pili kulia)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (kulia)
pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (kushoto), Mshauri wa Shamba la
Samaki la Ruvu, Per Gjoede (wa pili kushoto) baada ya kuhitimisha ziara
fupi ya mafunzo katika shamba hilo. Mkuu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)
nchini, Peter Malika akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam. Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour
akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku mbilli ya wadau wa mradi
wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Same, Rosemary Staki. Mkuu
wa wilaya ya Same, Rosemary Staki akitoa salamu kwa wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe wakati wa warsha
hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Ofisa
Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji katika Shirika la Umoja wa
Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Imanuel Muro akisimamia
majadiliano kuhusu wa kampuni ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani
Same mkoani Kilimanjaro wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi
wa ufugaji samaki kibiashara katika bwawa hilo iliyoandaliwa na UNCDF
na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mkiurugenzi
Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr. Charles Mhina
akitoa maoni kwenye warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa kijiji cha Misufini kata ya Ngungu wilaya ya Same, Omari Mganga
akiwasilisha maoni wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa kijiji cha Mgandu kata ya Bendera wilaya ya Same, Merina Mhando
akichangia maoni katika warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mtaalamu
wa Mawasiliano na Ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko
wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Jacqueline Namfua-Mwombela na
Mshirika wa Programu UNCDF, Andulile Mwabulambo wakifurahi jambo wakati
wa warsha hiyo iliyofanyika wmishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni washirki wa warsha ya siku mbili ya mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyoandaliwa na UNCDF na
kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment