Mbunge
wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) akioneshwa moja
kamba na mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan zinatokana
na zao la pamba katika kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho leo
Wilayani Igunga kata ya Choma. Katikati ni katibu wa kiwanda cha Nyuzi
Tabora. ( Picha zote na Raymond Urio )
Mmiliki
wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akizugumza na Mbunge wa
Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati), alipotembelea kuona
maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho leo Wilayani Igunga kata ya
Choma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Igombensabo Lazaro Ngullo .
Mbunge
wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akipewa moja ya maelezo ya
mashine ya ya zao la pamba ndani ya kiwanda cha Manonga Genery, leo
alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo
Wilayani Igunga kata Choma.
Mmiliki
wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akimpa maelekezo Mbunge wa
Manonga Seif Khamis Gulamali ndani ya kiwanda hicho (katikati), leo
alipotembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda kilichopo Wilaya
ya Igunga kata ya Choma.
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Igombensabo.
Mbunge
wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akiongozana na viongozi wa
serikali pamoja na wahandisi alipotembelea kiwanda hicho leo kilichopo
Wilayani Igunga kata ya Choma.
Mbunge
wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati) akisikiliza kwa
makini maelekezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery,
Urvesh Rajan leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda
hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.
Mbunge
wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akisaliamiana kwa furaha na
mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan leo alipotembelea
kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga
kata Choma.
NA RAYMOND URIO
Mbunge
wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis
Gulamali leo ametembelea kiwanda cha Manonga Ginery kinachohusika na
kutengeneza pamba, kilichokuwa kimesimama kwa takribani miaka ishirini
(20) bila ya kufanya.
Mapema
leo hii Mbunge Gulamali aliwasili katika eneo la kiwanda hicho, iliyopo
Jimbo la Igunga Kata ya Choma akiwa pamoja na Mmiliki wa kiwanda hicho,
ndugu Urvesh Rajan pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa, wahandisi
na mafundi wa viwanda.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya
ufufuaji wa kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi upya, baada ya kukaa
kwa miaka kadhaa bila ya kufanya kazi, Mbunge Gulamali alisema, leo
nimekuja kuoana maendeleo ya kufufuliwa wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu
ya kutaka kutimiza tena ahadi yangu niliyo itoa kwa wanachi wa Igunga
na Manonga kwamba lazima kiwanda cha Manonga Ginery, kianze kazi ili
wananchi waweze kunufaika katika zao biashara ya pamba na wengine kupata
ajira kwa kuendesha maisha na kukuza uchumi wa viwanda nchini.
"
Leo nimekuja kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hichi ikiwa ni
sehemu yangu ya ahadi niliyo itoa kwa wananchi wangu wa jimbo la Manonga
pamoja na Igunga kwamba lazima kiwanda hiki kifanye kazi tena, ili
biashara ya zao la pamba lirudi tena na wananchi na waweze kupata ajira
katika kiwanda hichi pia kukuza uchumi wa nchi ya Viwanda.
"
Kufufuliwa kwa kiwanda hiki ni fursa kubwa ya maendeleo kwa jamii ya
wana Igunga na Manonga na hasa wakulima wa zao la pamba hata kwa
wananchi wanao lilia ajira, hivyo fursa kwa sasa iko wazi, alisema
Gulamali.
Hata
hivyo Mbunge Gulamali alisema kuwa bila kumpa ujumbe mmiliki wa kiwanda
hiki na kutompa matakwa ya wananchi basi ingekuwa sicho kilichotokea
leo, kwahiyo nimetumia uongozi wangu kwaajili ya wananchi wangu ili
kuona maendeleo yakiendelea tena katika swala kiwanda na kuona zao la
pamba likirudi tenaa kwa kasi katika Jimbo la Igunga na Manonga.
Lakini
pia Mbunge Gulamali amewataka wakulima wa zao la pamba kuanza kulima
kwa kasi kilimo cha hicho kwa kuwa sasa kiwanda hiki kitaanza kufanya
kazi, hivyo juhudi na jitihada zenu ndio itakayoweza kufanya kiwanda
hiki kiendelee kwa kuwa nao wanategemea pamba toka kwenu na wao waweze
kuuza kwa wafanya biashara wakubwa wa nje ya mipaka na ndani ya nchi.
Hata
hivyo Mmiliki wa kiwanda hicho, ndug, Urvesh Rajan amemshukuru Mbunge
Gulamali sambamba na uongozi wa serikali wa kata ya Choma kwa kuweza
kuvumilia kwa kipindi chote tangia kiwanda kilivyo simama na hata pale
alitoa ombi lake la kukufua tena kiwanda waliweza kumsikilliza na hivyo
ni jambo la kushukuru.
Lakini
pia mmiliki wa kiwanda hicho ndug, Rajan ametoa ombi kwa wakulima wa
zao la pamba kuweza kujitaidi kulima zao hili kwa kasi, kwa kuwa kiwanda
kinategmea sana zao hili na si zao jingine, hivyo pesa watakayo ilipa
toka kwawakulima wana imani nao itarudi pale watakapo wauzia wafanya
biashara na ndio kiwanda kitazidi kuendelea.
"
Ninafurahi Mbunge Gulamali ameitikia wito wangu kwa kuja na kuona
maendeleo ya kutaka kufufua kiwanda hichi hivyo, ni jambo zuri kuona
kiongozi akiwa sambamba na wewe na mwenye kutaka maendeleo,
"
haitochukua muda tutaaenda kuanza kazi hivyo nina waomba wakulima wa
zao hili kuchangamkia fursa kwenye ulimaji kwa kuwa fedha watapata za
kuendesha maisha hata ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu,
alisema. Rajan.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa kijiji cha Choma, Ndug, Emmanuel Methew alisema
kuwa kitendo kilichofanyika leo cha mbunge kuja kuona maendeleo ya
ufufuaji wa kiwanda hiki ni kitu kizuri kutokana ni mikaa mingi
kutofanya kazi hivyo wakulima walikuwa wanapata tabu katika zao hili,
hata mwishowe kukata tamaa katika kulima zao hili kutokana na kufa kwa
kiwanda hiki.
"Kiwanda
kufufuliwa tena ni jambo zuri hivyo nina imani kuwa wakulima
watarudisha nguvu zao kwa kasi kwenye zao hili la pamba kwakuwa ndio
moja ya zao kubwa katika mkoa wa Tabora, alisema Methew.
No comments:
Post a Comment