Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea
Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es
Salaam (DDC).Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam
Sipora Liana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la
Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC)
wakati wa ziara yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko
Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI) George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi
kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la
Dar es Salaam (DDC) leo.
Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya
Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la
Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo
akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati
wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo. Katikati ni
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Baadhi
ya wajumbe wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es
Salaam(DDC) wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George
Simbachaweni(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi katika Mashirika
ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maenedeleo la Jiji la Dar es Salaam
(DDC).
Meneja
Mkuu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Hetson Msalale Kipsi akiwasilisha
taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene
(hayupo pichani) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la
Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC)
leo.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC), Rwandiko
Manumbu akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya yake kikazi
kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la
Dar es Salaam (DDC) leo.Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na baadhii ya wajumbe wa Bodi
za Mashirika ya Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) NA Shirika la
Masoko Kariako alipowasili katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam
leo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni akisalimiana na mmoja wa wafanyabiashara
katika Soko la Kariakoo Shimoni wakati wa ziara ya kikazi kutembelea
Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es
Salaam (DDC) leo.
Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kushoto) akimuongoza Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni(mwenye suti nyeusi) kuelekea katika Ofisi
za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara
ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo
leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na wafanyabiashara
wadogowadogo maarufu kama Machinga wanaopanga bidhaa zao mbele ya Ofisi
za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya
kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo
Jijini Dar es Salaam.
Picha zote: Frank Shija – MAELEZO
………………….
Nuru Juma – MAELEZO.
Serikali
imeipongeza Bodi na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji
la Dar es Salaam (DDC) kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo
richa ya changamoto wanazo kumbana nazo.
Pongezi
hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea
taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na
Shirika la Masoko Kariakoo alipokutana na menejinti ya mashirika hayo
leo.
Waziri
Simbachawene alisema kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika
nayo hivyo hana budi kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda
mfupi imeweza kufanya mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.
“Pamoja
na kuipongeza bodi hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo
mengine ya kuwekeza kama kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani
hilo ndilo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na
kuweka mahali ambapo watoto wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika
linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri
Simbachawene.
Simbachawene
alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa
taarifa nyingine itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.
Aidha
ameutaka uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuwa wabunifu kwa
kuanzisha masoko sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni
mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi na njia ya kuongeza ajira kwa
vijana.
Alilitaka
Shirika hilo kuachana na mawazo ya kizamani na badala yake wajipange
kimkakati ili kuendana na wakati ikiwemo kufikiria namna ya kuwaza
kushusha mizigo katika soko hilo kwani serikali haitaweza kuruhusu
maroli ya mizigo kufika katika soko hilo ili kupunguza ya kuepuka
msongamano katikati ya jiji.
Aliushauri
uongozi huo uandae mikakati ya kuwezesha soko hilo kuwa la kiwango cha
juu (Super Market) na kuwalipisha wafanyabiashara kiwango kinachoendana
na bei halisi ya soko kama ambavyo wapangishaji wengine wamekuwa
wakitoza ili kukuza kipato kwa Taifa.
Waziri
Simbachawene ameahidi kushirikiana na mashirika hayo katika kutatua
changamoto ambazo zinahitaji msaada wa uongozi na kuwataka wafanye kazi
kwa bidii kwani Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji watu wanaojituma na
kuchapa kazi.
Awali
akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es
Salaam Meneja Mkuu wa Shirika hilo Rwandiko Manumbu alisema kuwa pamoja
na changamoto wanazokumbana nazo Shirika limefanikiwa kutoa shilingi
milioni 140/- kama gawio kwa mwanahisa wake ambaye ni Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam.
“Mhe.
Waziri, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Shirika hili tumeweza
kutoa gawio la kiasi cha shilingi milioni 140/- kwa Halmashauri ya Jiji
na haya ni mafanikio makubwa kwetu,” alisema Manumbu.
Kwa
upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita
amempongeza Waziri Simbachawene kwa utayari wake wa kushughulikia
changamoto zinazo yakabli mashirika hayo ikiwa ni pamoja na kutenga muda
wake kuja kusikiliza matatizo yao.
Pamoja
na pongezi hizo Mwita alishauri Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam
(DDC) kuangalia uwezekano wa kurejesha bendi za muziki kama ambavyo
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyokuwa amedhamiria
wakati wa uanzishwaji wa Shirika hili.
Shirika
la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko
Kariakoo ni mashirika ya Umma yanayoongozwa na Serikali kupitia
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Sheria za Makampuni namba
2012 ya mwaka 1971 na Sheria ya Bunge namba 36 ya mwaka 1974, “The
Kariakoo Market Corporation Act, 1974
No comments:
Post a Comment