Wajumbe
wa Bunge la Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola wakiwa katika picha ya
pamoja kabla ya kuaza kwa Mafunzo ya wiki moja yalioandaliwa na Bunge
hilo, katika mafunzo hayo Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
limewakilishwa na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson na Baraza la Wawakilishi
Zanzibar limewakilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe
Simai Mohammed Said.
Naibu
Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson pamoja na Mwakilishi wa
Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said wakishiriki katika masomo ya wiki
pamoja huko Afrika Kusini University of Wits ambapo jumla ya Wabunge
kutoka nchi 16 kutoka Jumuiya za Madola wameshiriki masomo hayo.
Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwasilisha kazi
ya kikundi wakati wa mafunzo hayo ya wiki moja yanayofanyika Nchini
Afrika Kusini yalioandaliwa na Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola,
akieleza kuhusiana na umuhimu wa kamati za kudumu za mabunge ya Jumuiya
Madola kuelekea karne 21.
Kutoka
kushoto ni Mbunge kutoka India Ajay Misra, Naibu Spika Tanzania Dr
Tulia Ackson, Seneta kutoka Jamaica Charles Pearnel na Mussa Dlamini
Swaziland. Masomo hayo yanafanyika Johanessberg University of
Witwatersrand kwa wiki moja na kudhaminiwa na Commonwealth Wealth.
Wawakilishi
kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Naibu Spika Dr.Tulia
Ackson pamoja Simai Mohammed Said kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar
wakiwa masomomi South Africa University of Witwatersrand wakibadilishana
mawazo na Mbunge wa Swaziland Mhe Mussa Dlamini
Naibu
wa Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson akisikilizwa kwa umakini
na washiriki wenzake. Kutoka kushoto Mhe.Simai Mohammed Said ( Zanzibar
) Pearnel Charles Junior ( Jamaica) Mussa Dlamini ( Swaziland ) na Ajay
Misra ( India).
Waheshimiwa
Wabunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola wakiwa katika mafunzo Nchini
South Africa. wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.
Wajumbe
kutoka Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ( Commonwealth Countries)
wakitembelea Mahakama ya Katiba ( Constitutional Court ) katika mji wa
Johannesburg.
Mwakilishi
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai
Mohammed Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa
mafunzo hayo kutoka kushoto Mbunge wa Jamaica.Mhe.Heroy Clarke ( MP),
Charles Pearnel Seneta pia akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Jamaica,
Stewart Michael ( MP) na Victor Wright ( MP ).
Mjumbe
kutoka Jumuiya ya Madola pia akiwa Mwakilishi kutoka Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akibadilishana mawazo na
Profesa David Everatt ambaye ni Kiongozi wa Skuli ya Utawala katika
University of Wits, South Afrika.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Tulia Ackson akitoa
nasaha zake za shukrani kwa niaba ya Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya
Madola walioshiriki mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa
University of Witwaterstrand, Johannesburg South Africa.
No comments:
Post a Comment