Mtendaji wa Mtaa wa Pangani, Kata ya
Kati Bi. Maria Singo
akichangia hoja kwenye kikao kazi kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa kwa ajili ya
kuhamasisha ukusanyaji wa kodi ya Mapato.
Nteghenjwa Hosseah, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewaagiza watumishi wa
Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiana na watumishi wa Mamalaka ya
Mapato Tanzania(TRA) Mkoa kukusanya Tsh Bilioni moja za kodi ya majengo kwa
kipindi cha Mwezi wa Nne.
Rc Gambo ameyasema hayo wakati wa kikao kazi na watendaji wa
Kata, Mitaa, Wahasibu wa Mapato, wataalamu wa Mipango Miji pamoja na watumishi
wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Arusha kilichofanyika mapema wiki hii.
Akizungumza katika Kikao hicho cha kuangalia namna ya
kukabiliana na changamoto ya kutokusanyika kwa Kodi ya Majengo kwa mwaka wa
Fedha 2016/2017 Rc Gambo amesema hata kama hata kama chanzo hicho kimehamishiwa
TRA, Halmashauri ya Jiji bado ina mchango mkubwa katika kufikia Malengo
yaliyowekwa kwa kushirikiana na wataalamu wa TRA kwenye Kata na Mitaa yote ya Jiji.
Aliongeza kuwa Jiji kuna watumishi wengi ambao wanafahamu
kila nyumba katika mitaa yote ya Jiji na wamekuwa wakifanya kazi hii kwa
kipindi kirefu hivyo wana uzoefu wa kutosha na ushiriki wao katika kipindi hiki
cha kuelekea mwisho wa mwaka wa Fedha ni muhimu sana ili kwa pamoja tuweze
kufanikiwa kukusanya maduhuli ya Serikali kwa ufanisi.
Alisema maeneo yote ambayo hayajapimwa kila mmiliki wa jingo
atalipia Tsh 15,000 na maeneo ambayo hayajapimwa ila yamefanyiwa Uthamini
watalipa kwa kiwango walichokadiriwa na kwa maeneo yaliyopimwa ya kwa viwango
vya juu tunaangalia utaratibu mzuri wa kukusanya hivyo kila mmiliki wa jingo
atomize wajibu wake kwa kulipa kodi hii.
“Hapa tunachohitaji ni kuunganisha nguvu ya pamoja ili tuweze
kufikia Malengo na sio kwa sababu Chanzo hiki kiko chini ya TRA kwa sasa basi
Jiji basi Taasisi zingine zisitoe Ushirikiano mimi kama Msimamizi wa shughuli
za Serikali ntashirikisha kila Taasisi inayohusika ili kufanikisha Malengo ya
ukusanyaji na sio katika chanzo hiki tu bali katika Vyanzo vyote alisema Gambo”.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro
amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba kazi hiyo itafanyika kwa kadiri ya
Maelekezo waliyoyapokea na kwamba ana imani kubwa na wataalamu wa Jiji kwa kuwa
wamekwishashiriki mazoezi kazi
mbalimbali na kuleta mafanikio makubwa katika Wilaya hii.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia aliongeza
kuwa atawasimamia watendaji ipasavyo katika kukusanya kodi ya Majengo na
ataendelea kuwajengea uwezo ili kuongeza ufanisi katika zoezi hilo.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Arusha, Apili
Mbarouk ameelezea hali ya ukusanyaji wa chanzo hiki kwamba hairidhishi kwani
mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya Tsh Mil 200 tu wakati malengo ya Ukusanyaji
wa mwaka wa Fedha unaoishia Juni 2017 ni Tsh Bil 5 hivyo ni vyema kuongeza
nguvu ili kufikia Malengo.
Kikao kazi hiki ni muendelezo wa wa Vikao vinavyoitishwa na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Gambo katika
kutatua kwa pamoja changamoto za sekta mbalimbali katika Mkoa huu ili kuleta
Mafaniko ya pamoja.
|
No comments:
Post a Comment