MWENYEKITI
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni
wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini.
Katika
hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena,
wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa
Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na
mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro.
Akizungumza
kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi
alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha
shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza.
Alisema
jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu
wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa
kwa ujumla.
- Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)
“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili.
Aidha
alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa
kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki
mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia.
Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi.
Aliwatakia wageni wake chakula chema.
Mgeni
rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema
kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye
anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano.
“ …Business and friendship goes Together..” alisema
balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na
chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si
wa kubahatisha unakua.
Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika.
- Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
- Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi 'Application' ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville.
- Meza kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.
Post a Comment