Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto)
akimkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Charles Kichere kulia alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo
Mnazi Mmoja mapema leo asubuhi.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) akiweka
sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji yaliopo mnazi mmoja katika ziara zake baada ya
kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoji kutoka kulia ni
Naibu Kamishna Billy Mwakatage, Kaimu Kamishana Usalama dhidi ya moto
Fikiri Salla, Mhasibu Mkuu Chakala, Kaimu Kamishna wa Operesheni
Christom Manyologa na Kamishana Msaidizi Hamadi Muhando wakimfuatilia
kwa karibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles
Kichere hayupo pichani, alipofanya ziara katika Jeshi hilo mapema leo
asubuhi tarehe 06/04/2017
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto)
akimfuatilia kwa karibu huku akiandika, Kamishana MKuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, Kamishna huyo aliambatana na
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo (kulia)
alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo Asubuhi.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto)
akimpatia zawadi ya Kalamu ya Jeshi yenye namba ya dharura 114, Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) mapema
leo asubuhi alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo
asubuhi.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto)
akimsindikiza Kamishana MKuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles
Kichere (kulia) akiondoka Makao Makuu ya Jeshi hilo alipofanya ziara
Mapema leo Asubuhi.(Picha Na Konstebo Joyceana Benson)
No comments:
Post a Comment