Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Rais John Pombe Magufuli alipongia madarakani alitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari.
Taasisi
ya Haki Elimu ni moja ya taasisi ambayo imefanya utafiti katika swala
la elimu na kuja na majibu ambayo yameonesha kuwepo kwa mafanikio
makubwa katika swala hili la elimu bure.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,Mkurugenzi
Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage ametaja kuwa tafiti hiyo imebaini
kuwa Sera ya elimu bila malipo imesababisha ongezeko la wanafunzi wa
darasa la kwanza hasa kwa shule za msingi.
“kulikuwa
na ongezeko la asilimia 43 na asilimia 10 kwa shule za Sekondari ,hali
iliyosababisha msongamano madarasani na pia kuongezeka kwa uwiano wa
mwalimu kwa mwanafunzi kwa darasa la kwanza hadi kufikia mwalimu mmoja
kufundisha wanafunzi 164 kwa wastani badala ya wanafunzi 45 wanaotakiwa”
amesema Kalage.
Amesema
kuwa utafiti huo ambao ulifanyika Wilaya za Njombe ,Mpwapwa ,
Sumbawanga ,Kilosa , Korogwe ,Tabora Mjini na Muleba kwa kuhusisha shule
28 na Msingi na 28 za Sekondari.
Amesema
kuwa utafiti umebaini kuwa shule zenye wanafunzi wachache kati ya
wanafunzi 200-300 zinapatiwa wastani wa Tsh 100,000-150,000 kwa mwezi
ambayo hutatua matatizo ya msingi kama ukarabati hasa kuzingatia fedha
za ruzuku zinatumwa shuleni kila mwezi.
Kalage
amesema tafiti hiyo imetoa mapendekezo kwa serikali,ifanye jitihada za
makusudi kuhakikisha kwamba wadau wote wanao elewa vizuri sera ya elimu
bila malipo ili kurahisisha utekelezaji wake .
Amesema
kuwa wadau wote wanapaswa kuzielewa nyaraka zote na miongozo kuhusiana
na sera hii ili kila mdau atambue wajibu wake na jinsi anavyopaswa
kushiriki katika utekelezaji wa elimu bure .
Amesema
kutokana na elimu kuongeza kwa uandikishaji wa darasa la kwanza
serikali ichukue hatua za makusudi kushughulikia changamoto
zitakazotokana na elimu bila malipo kama vile ongezeko la wanafunzi ,
uhaba wa madarasa , walimu , Vitabu na Vinginevyo.
Ametaja
kuwa zoezi la kupeleka fedha za ruzuku liende sambamba za serikali
kutoa fedha za maendeleo kwa ajili yakuboresha miundombinu ya shule
kwani shule nyingi zinachangamoto ya miundombinu na hivyo ni muda
muafaka kwa serikali kuanza sasa kusaidia shule kwa kuzipa fedha za
maendeleo kama amabvyo ilifanya wakati wa utekelezaji wa MMEM na MMES.
Mkurugenzi
wa Haki Elimu nchini , John Kalage akizungumza na wadau mbalimbali
wakati wa hafla ya uzinduzi wa tafiti juu ya mpango wa elimu bure
nchini.
Aliyekuwa
Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha
Qorro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya elimu bure
iliyofanyiwa utafiti na tasisi ya Haki eleimu nchini
Baadhi ya washiriki wakisikiliza ripoti hiyo kwa makini
Dr. Richard Shukia kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Elimu na Saikolojia akitoa maelezo juu ya tafiti hiyo
Wadau wakifatilia kwa makini maelezo kutoka kwa mtafiti
No comments:
Post a Comment