Pages

August 26, 2016

KIWANDA CHA SARUJI TANGA (SIMBA CEMENT) YATOA TANI 30 ZA SARUJI KWA ASASI YA KIRAIA

 Tangakumekuchablog
Tanga, KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, kimetoa tani thalathini za mifuko ya saruji kwa Asasi ya Kiraia ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya wazee.


Msaada huo umekuja baada ya Asasi hiyo kutuma maombi kiwanda cha Cement kufuatia kutokuwa na jengo ambalo litawahifadhi wazee hao na kuwapatyia huduma mbalimbali za Kiutu ambapo kwa sasa wamekuwa wakitoa kwa kuwafuata majumbani jambo ambalo limekuwa gumu kumfikia huduma kila mmoja.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiani leo, Injia wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Benedict Lema alisema sera moja ya kiwanda hicho ni kusaidia huduma muhimu za Binadamu.
Alisema wamekuwa wakitoa msaada kwa vituo vya Afya majengo ya shule pamoja na vifaa yakiwemo madawati.


Alisema msaada  huo kwa Asasi hiyo utasaidia kuendeleza jengo hilo ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi kwa wazee hao.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tushikamane Pamoja Foundation, Rose Mwapachu, alisema msaada huo umekuja muda muafaq na kusema kuwa utatumika kama ilivyokusudiwa.


Alisema wamekuwa wakiwahudumia wazee kwa kuwapitia majumbani kwao jambo ambalo limekuwa kero na gumu.


Alisema huduma hizo hazifanyiki kwa weledi hivyo kwa msaada huo watawakusanya mazee hao na kuwaweka pamoja na kuwapatia huduma zinazohitajika.






Mkuu wa fedha kiwanda cha Saruji cha Tanga (Sima Cement), Pieter Jaggar akimkabidhi mifuko ya Saruji 600, mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) ya jijini Dar es Salaam , Rose Mwapachu kwa ujenzi wa nyumba ya wazee .


  Injinia kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Benedict Lema, akimkabidhi mifuko ya saruji 600 Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya  Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) ya jijini Dar es Salaam, Rose Mwapachu, kwa ujenzi wa nyumba za wazee.




 Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement) Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya saruji 600 mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Tushikamane Pamoja  Foundation (TPF)  , Rose  Mwapachu kwa ujenzi wa nyumba ya wazee.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...