Baadhi
ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye
ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye
maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe
Yanga Dar es Salaam leo mchana.
Bango likihimiza kuungana kutokomeza homa ya ini.
Maandamano
yakiendelea kuelekea viwanja vya Mwembe Yanga. Katikati ni Mratibu wa
Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan.
Vijana waliopo kwenye mtandao wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan, akizungumza kwenye maadhimisho hayo. |
Mwenyekiti wa TanPud Tanzania, Godfrey Ten, akizungumza katika maadhimisho hayo.
Ofisa
Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa Asasi za Kiraia kutoka Tume ya Kuratibu
Udhibiti wa Dawa za Kulevya Tanzania, Salome Mbonile, akizungumza kwenye
maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa Taasisi ya Pasada, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu
wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo
akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo.
Maadhimisho yakiendelea.
Vijana waathirika na dawa za kulevya wakicheza kwenye maadhimisho hayo.
Meneja wa Afya Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde akizungumza kuhusu ugonjwa huo.
Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.
Dotto Mwaibale
UGONJWA
wa homa ini umepangwa kutokomezwa ifika mwaka 2030 imefahamika ambapo
watu wapatao milioni 1.4 upoteza maisha ulimwenguni kutokana na
maambuki ya ugonjwa huo ulimwenguni hasa kwa wale wanaotumia mihadarati
kwa njia ya kujidunga.
Hayo
yalibainishwa na Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya
Temeke, Mwajuma Mwihumbo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini
yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana.
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufahamu kuhusu na kuungana na juhudi za ulimwengu za kutokomeza homa ya ini.
Alisema mada ya kampeni ya kimataifa ya homa ya ini ya mwaka huu ni utokomezaji ambao ni mwaka muhimu kwa homa ya ini.
Alisema
lengo la maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia,
wafanyakazi wa huduma za afya, taasisi na vikundi vya utetezi na
ushawishi ni kuongeza ufahamu wa homa ya ini B na C hasa kwa makundi
hatarishi kama watumiaji wa mihadarati wanaojidunga.
Meneja
wa Afya Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya
Medicins Du Monde alisema katika mkutano mkuu wa 69 wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) ni serikali zote ziliazimia kwa pamoja kuidhinisha mkakati
wa ulimwengu wa utokomezaji wa homa ya ini.
Alisema
hadi Februari 2016 nchi 36 zilikuwa zina mipango ya kitaifa ya
utokomezaji wa homa ya ini na nchi 33 zipo katika mikakati ya kuandaa
mipango hiyo.
"Mkakati
unalenga kutokomeza homa ya ini B na C ifikapo mwaka 2030 ambapo
unahusisha malengo ya tiba ambayo iwapo yatafikiwa yatapunguza vifo
vinavyosababishwa na homa ya ini kwa asilimia 65 na kuongeza huduma ya
tiba kwa asilimia 80 hivyo kuokoa maisha ya watu milioni 7.1 ifikapo
mwaka 2030" alisema Dk. Aikaeli
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
No comments:
Post a Comment