Kiongozi
wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis ameteleza na kuanguka alipokuwa
akielekea kwenye altare kuongoza ibada ya misa nchini Poland.
Inaelezwa kuwa alikosea kukanyaga ngazi huku amelikanyaga vazi lake la
misa.
Mapadre
waliokuwa karibu naye walikimbia na kumsaidia kuinuka. Misa iliendelea
kama ilivyopangwa na papa alihubiri kwa muda mrefu mbele ya maelfu ya
waumini waliokusanyika Jasna Gora katika jiji la Czestochowa, kusini mwa
nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment