Pages

July 10, 2015

MICHUANO YA MBATIA CUP 2015 SASA YAMALIZA HATUA YA KWANZA YA KUPATA MABINGWA WA KATA

Kikosi kamili cha timu ya Wazalendo kabla ya mchezo wa fainali.
Kikosi kamili cha Himo fc kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali .
Katibu Mwenezi wa chama cha NCCR -Mageuzi ,Stanley Temba akiwa ameongozana na katibu wa Vijana wa chama hicho katika jimbo la Vunjo  Danieleson Shayo wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali.
Waamuzi wa mchezo huo,Kabwe Korona,Beda Lyimo na Nassib wakizungumza na manahodha wa timu hizo.
Benchi la ufundi la timu ya Wazalendo likongozwa na raia wa Kigeni.
Heka heka ndani ya uwanja .
Baadhi ya Mashabiki waliofika kushuhudia mchezo huo wa fainali.
Mmoja wa Shabiki wa timu ya Himo fc ,Mzee Rashid aliyekuwa kiutio katika mchezo huo hasa kutokana na midadi aliyokuwa nayo wakati mchezo ukiendelea.
Mchezo huu ulikuwani burudani kwa wakazi wa mji wa Himo wa jinsia zote.
Huyu hakuweza kufahamika mara moja kama alikuwa ni Shabiki wa moja ya timu zilizokuwa zikicheza.
Licha ya mchezo kuendelea bado uwanjani kulionekana kuwepo kwa kuku wakiendelea kutafuta chakula.
Hata hivyo mchezo huo uliingia Dosari baada ya kutokea kwa vurugu zilizopelekea mchezo kuvunjwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...