Hawa mashabiki wa Manny Pacquaio hawakujua kama mwisho wa pambano ingekuwa hivi, na walikuwa na uhakika kwa asilimia zote kwamba ni lazima Pacquiao angeshinda.
Lakini mwisho wa siku matokeo yaliamua kuwa Floyd Mayweather ndiye mbabe kwa mwanzake Manny Pacquiao baada
ya pambano la raundi 12 ambapo Mayweather alimshinda Pacquiao kwa
pointi sita akiwa na pointi 117 huku mwenzake akiwa na 111.
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali huko Ufilipino
waliacha kazi zao kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo katika maeneo
mbalim,bali ya wazi kkwenye Screen kubwa katika pambano lililokuwa
likipigwa Las Vegas, Marekani.
Ukiachia
Ufilipino mashabiki walijitokeza isivyo kawaida kila pande duniani na
kila mmoja alikuwa na uhakika na ushindi wa mtu anayemkubali kati ya
mastaa hao wawili duniani.
No comments:
Post a Comment