Pages

May 4, 2015

MZIIKI KWA KUSHIRIKIANA NA VODACOM TANZANIA YANOGESHA ZARI ALL-WHITE PARTY

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiimba jukwaani Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea wateja burudani ya muziki kiganjani. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.
Mchumba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinum... Bibie Zari the bossylady akiwashukuru Watanzania waliofika katika Zari White Party lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Umati wa Watanzania waliohudhuria katika Zari White Party lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja ya vingozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akitoa maelezo machache kwa wateja waliofika katika Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. App hiyo inawaletea wateja burudani ya muziki kiganjani.
Msanii wa Kizazi Kipya, Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi akipozi katika zuria jekundu.
Msanii Shetta nae hakuwa nyuma kushow love mbele ya zuria jekundu.

Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa amepozi katika zuria jekundu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinumz ambaye ni balozi wa Mziiki ambayo ni program ya simu za mkononi (mobile app) ya Vodacom Tanzania akiwa amepozi na mkewe mtarajiwa Zari katika Zari White Party iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Waliopo pembeni ni Madame Ritha, Msanii Ney Wa Mitego. Wengine ni Msanii A.K.A (kushoto) toka nchini Afrika Kusini.
---

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...