Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiendesha
mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari
yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini
ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Na Mwandishi Wetu, Sengerema
AWAMU
ya pili ya mradi wa kuwezesha redio za jamii kuhamasisha wananchi
kushiriki katika kilimo, afya na elimu unatarajiwa kuanza Julai mwaka
huu baada ya awamu ya kwanza ya miaka mitatu kuonesha mafanikio makubwa.
Kauli
hiyo imetolewa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al
Amin Yusuph, wakati akihojiwa kuhusiana na mafunzo ya Tehama kwa
Mawakala wa habari wa Redio za Jamii nchini yanayofanyika mjini hapa.
Alisema
japo mradi huo umemalizika, kumekuwepo na mabadiliko mengi katika
uendeshaji wa redio hizo za jamii ikiwa ni pamoja na matumizi ya Tehama
katika kutengeneza vipindi na kuvirusha.
Mradi
huo wa uwezeshaji wa miaka mitatu ulimalizwa kwa mafunzo ya siku nne
katika kituo cha redio jamii cha Sengerema Telecentre ambapo washiriki
kutoka redio 9 walijifunza matumizi ya teknolojia katika kutengeneza
vipindi, kukusanya taarifa kwa kutumia simu za kawaida na namna ya
kuendesha redio hizo kuwa na mvuto na kutengeneza mpango kazi wa
biashara.
Mradi
huo unaofadhiliwa kwa pamoja na Unesco na shirika la maendeleo la
Sweden ( SIDA) limelenga kumwezesha mfanyakazi wa redio kutumia simu za
mkononi kukusanya na kuboresha habari zake na kuzituma katika redio kwa
matumizi ya ushawishi.
“Tumeona
mafanikio makubwa kwani kwa sasa wawakilishi wa redio hizi wanaweza
kutengeneza vipindi kwa kuwashirikisha wanavijiji kutoa sauti zao ili
zisikike,” alisema kutokana na hilo redio hizo sasa zimekuwa maarufu na
za kuaminika.
Alisema
nia ya Unesco ni kuhakikisha kwamba redio hizo zinashiriki kikamilifu
katika kuhakikisha wananchi wanatoa na kupata taarifa zinazoweza
kutumiwa na redio hizo kuhamasisha shughuli mbalimbali zikiwemo za
kiafya, kielimu na kilimo.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akitoa
maelekezo kwa vikundi kazi wakati mafunzo hayo.
Miongoni
mwa washiriki wa semina ya mwisho Pili Mlindwa wa redio jamii ya Panga
FM akizungumzia mafunzo waliyopewa katika matumizi ya Tehama, alisema
yamembadili sana katika utendaji wake na kumuongezea maarifa ya kazi.
Alisema
amefurahishwa sana na mafunzo ya Tehama ambayo sasa anaweza akafanya
kazi nje ya studio na bado mhariri wake akawa na taarifa yake na
kuitumia.
Alisema
mafunzo mengi aliyopata katika mradi huo yakiwemo pia ya matumizi ya
meseji Matrix, simu za mkononi kukusanya na kutoa taarifa kumemfanya awe
wa kujiamini.
Naye
mwandishi wa habari, Bakari Khalid wa redio jamii Kaham FM ya Shinyanga
akizungumzia Mafunzo ya Tehama alisema kwamba Unesco imefanya jambo la
maana kuwapa mafunzo hayo ikizingatiwa kwamba redio nyingi zina watu
wasiopitia chuo.
Alisema kwa sasa wanaweza kutengeneza vipindi bora vya kuhamasisha afya, elimu na kilimo na namna ya kuandika habari.
Aidha alisema sasa wana uwezo wa kutumia kompyuta mpanguso (tablet) katika kuandaa vipindi na pia kuandaa taarifa mbalimbali.
Wakala
wa habari wa kituo cha Orkonerei Radio Service (ORS) cha wilayani
Simanjiro, Nyangusi Ole Sangida akichangia mada kuhusu changamoto
zinazowakabili Mawakala wa Redio Jamii katika ukusanyaji wa habari
wakati wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea
habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza
chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa
ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni
(UNESCO).
Wakala
wa habari wa kituo cha redio jamii Pangani FM, Pili Mlindwa akichangia
mada wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku nne ikiwa ni sehemu ya mradi
wa SIDA wa kuwajengea uwezo katika kuwawezesha kutengeneza vipindi bora.
Wakala
wa habari wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Paulina Juma
akiwasilisha kazi ya kikundi ya kuandaa habari na kurekodi kipindi
waliyofanya kwa vitendo katika Kompyuta mpanguso (Tablet) walizokuwa
wakitumia kwenye mafunzo hayo.
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki
wa mafunzo hayo.
Baadhi
ya mawakala wa habari wa vituo vya redio jamii wakifanya mafunzo kwa
vitendo kwa kutumia Kompyuta mpanguso (Tablet) wakati wa mafunzo ya
matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na kupokea habari yaliyofanyika
katika kituo cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa ushirikiano na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Baadhi ya mawakala wa habari kutoka vituo mbalimbali va redio jamii nchini wakiwa katika za vikundi.
Wakala
wa habari wa kituo cha Redio Jamii Pambazuko FM, Kaima Akida akifanya
"Recap" ya mafunzo yaliyokuwa yakiendeshwa na Ofisa Miradi ya
Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (hayupo pichani).
Mshauri
na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza machache wakati wa
kufunga mafunzo ya siku nne kwa mawala wa redio jamii nchini ambapo
aliwaasa kuyazingatia na kuyafanyia kazi waliyojifunza pindi warudipo
kwenye vituo vyao vya kazi. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano,
Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Wakufunzi
na washiriki wa mafunzo ya matumizi ya kutumia TEHAMA kwa kupeleka na
kupokea habari yaliyofanyika katika kituo cha Sengerema Telecentre
mkoani Mwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA)
kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni (UNESCO).
No comments:
Post a Comment