UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA WASHEREHEKEA MIAKA 51 YA UHURU
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Aziz Ponary Mlima akiwa na mkewe Mama Mkola Mlima pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi wakiwapokea wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliandaa sherehe fupi kuuenzi Muungano.
Balozi Mlima akitoa hotuba fupi wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Balozi Mlima akikata keki kuadhimisha miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anayeshuhudia ni Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ambaye ni Naibu Waziri wa Biashara ya Kimataifa na Viwanda wa Malaysia, Seneta Deto' Lee Chee Leong.
Juu na Chini ni Wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Mlima (hayupo pichani) alipowahutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
No comments:
Post a Comment