Pages

May 6, 2015

MEYA MWENDA WA KINONDONI ASHINDA TUZO YA MEYA BORA AFRIKA

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola ‘President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award’ ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.

Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu.

Tuzo hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo za MajijiMadogo (Small Size Cities).

Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya Cape Verde.

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya (Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).

Miradi iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA.

Zawadi zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200.

Majiji mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana. Mwingine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mbando na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty pamoja na watendaji wengine wakifuatilia kwa makini wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa amenyanyua Tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Marekani 100,000 kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kumkabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA) kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...