Pages

May 5, 2015

Mbowe Apokelewa Kwa Shangwe Na Madereva Waliogoma Ubungo, Waokoa Jahazi na Mgomo Kwisha


Leo tena hali ikawa kama jana, daladala na mabasi makubwa ya kwenda mikoani yote yaliendeleza mgomo.. ikafika saa sita mchana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakaongea na viongozi wa Chama cha Madereva wakakubaliana na baadae mgomo ukaisha mabasi yakaanza safari. Jahazi limeokolewa na viongozi hawa ambapo DC Makonda amewaahidi kwamba ameunda Tume ambayo itakutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kupata tamko la Serikali kuhusu madai ya madereva hao, na majibu yatapatikana kesho asubuhi kutoka Serikalini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...