Freeman Mbowe akizungumza na madereva |
PICHANI NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRSIA NA MAENDELEO FREEMAN BOWE AKIZUNGUMZA NA MADEREVA MBALIMBALI UBUNGO
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Mh FREMAN MBOWE
amewasili jana katika kituo cha mabasi Ubungo kuzungumza na madereva ambao
walikuwa wakiendelea na mgomo wa kuitaka serikali iwasikilize shida zao,
Mbowe ambaye aliwasili hapa majira ya saa nne kasoro asubuhi alijikuta
katika wakati mgumu baada ya wananchi kumshangilia kwa nguvu huku
wengine wakifuta barabara ili gari yake ipite huku nyimbo za Ukawa
zikiimbwa,jambo ambalo lilizua taharuki katika eneo hilo.
Mh mbowe
alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa madereva hao.
Kuhusu mgomo huo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh PAUL MAKONDA amewaomba
madereva hao kuendelea na kazi na ndani ya siku saba serikali itakua
tayari imeshatoa tamko.
Madereva hao wamekubali kuanza safari kwa sharti la ndani ya siku saba
wawe wamesikilizwa kero zao.MH MBOWE alipotaka kuzungumza na madereva hao
microfone zote zilizimwa na kufichwa kusikojulikana jambo ambalo
lilifanya ashindwe kusikika kwa madereva hao na kuamua kumtoa nje na
kusukuma gari yake hadi maeneo ya Shekilango na kurudi ofisini.Taarifa
ni kuwa mgomo huo umekwishwa na magari hapa ubungo yameanza kutoka.
Chanzo;Matukio na Vijana
No comments:
Post a Comment