Tetemeko
kubwa la ardhi limekumba eneo lililo Magharibi mwa Nepal karibu na Mji
Mkuu wa Kathmandu .Maafisa wa polisi wamethibitisha kuwa zaidi ya watu
560 wamefariki dunia huku wengi wakiwa hawajulikani waliko na kwamba
huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Shirika
la utafiti la Marekani limesema kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9
lilikumba eneo lililo umbali wa kilomita nane Mashariki mwa Pokhara
Magharibi mwa mji Mkuu wa Kathmandu.Kuna ripoti za uharibifu wa majengo
na bidhaa, makazi ya watu hata miundo mbinu ya Mawasiliano ya simu nayo
yameharibiwa vibaya.
Picha za majengo yaliyokuwa yameporomoka pamoja na mahekalu ya miaka mingi iliyopita zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii.
Walioshuhudia walisema kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.
Mitetemeko mingine midogo imesikika kaskazini mwa India pamoja na nchini Pakistan.
-BBC
No comments:
Post a Comment