Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,
akizungumza na halaiki ya vijana wa chama hicho muda mfupi baada ya
kuifunga kambi ya mafunzo ya vijana hao iliyofanyika Kijiji cha
Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.
Mamia ya
wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wakimshangilia Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (hayupo
pichani), katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule
ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo juzi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,
akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya
Itilima mkoani Simiyu juzi.
Wazee wa
kabila la wasukuma wakimuombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ili yeye na chama
chake aweze kutawala nchi. Mbowe alisimikwa na kupewa zana za kitemi za
kabila hilo na kuitwa jina la Mayego kabla ya kuanza kuhutubia mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima
mkoani Simiyu juzi.
No comments:
Post a Comment