Mratibu wa maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Muungano kutoka EAC,Maganya Fadhil akizungumza katika hafla hiyo. |
Baadhi ya wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)wanaounda Umoja wa Watanzania wakifatilia tukio hilo. |
Mwenyekiti
wa Umoja wa Watanzania wanaofanyakazi EAC,James Kuleiye akishuhidia
ukataji wa Keki uliokuwa ukifanywa na watumishi wenzake,Maria Ruhere na
Luis Pascal. |
Uongozi wa hospitali wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi hao. |
Filbert Rweyemamu,Arusha |
Press ? for Keyboard Shortcuts.
Umoja
wa Watanzania wanaofanyakazi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki(WATJAM)yenye makao yake makuu jijini Arusha katika
kuhadhimisha Sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo
wametembelea hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru kufanya usafi
na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 3.7
milioni
Mwenyekiti
wa umoja huo,James Kuleiye amesema wao kama watanzania wameona waitumie
siku ya leo kufanya shughuli za kijamii na kuwa karibu na taasisi hiyo
kwa lengo kujenga mahusiano mema.
Misaada
iliyotolewa ni Maji maluumu ya wagonjwa ,Mashuka 50,Vifaa tiba vya
kupima mapigo ya moyo(Presha) na vifaa mbalimbali vya usafi.
Mganga
Mkuu wa hospitali hiyo,Aziz Msuya ameshukuru umoja huo kwa moyo wa
uzalendo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo licha ya kueleza
changamoto inayoikabili hospitali hiyo ya kutokuwa na Wodi ya kuwalaza
wagonjwa waliofanyiwa Upasuaji.
Amesema
vifaa hivyo vitakua msaada mkubwa kuboresha afya ya mama na mtoto kwani
kila mwezi jumla ya wanawake 300 hujifungua huku 50 wakijifungua kwa
upasuaji.
Picha na habari zimeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment