Pages

April 26, 2015

LUCAS Kadawi Limbu, mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha ACT-Tanzania amtuhumu Msajili wa vyama vya Siasa

Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,Lucas Kadawi Limbu
LUCAS Kadawi Limbu, mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha ACT-Tanzania, ameibuka na kumtuhumu Msajili wa vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuingilia mwenendo wa kesi ya madai dhidi ya Zitto Kbawe na genge lake.

Aidha, Limbu anatuhumu Jaji Mutungi kuwabeba “wahalifu waliovamia chama chake, kukibadilisha nembo, kadi na katiba.” Anaripoti Pendo Omary … (endelea).

Limbu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jumapili kuwa kitendo cha msajili cha kuruhusu ACT-Tanzania kubadilishwa jina, ni kuingilia uhuru wa mahakama na kutoa maamuzi nje ya mahakama.

Anasema, “Huyu ni Jaji wa Mahakama Kuu. Amewahi kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa na hakimu wa mahakama ya mkoa. Anajua taratibu, kwamba kuna kesi mahakamani na hivyo, siyo sahihi kuupa upande mmoja haki, wakati shauri halijaamuiriwa.”Kauli ya Limbu imefuatia tamko la msajili la Ijumaa 24 Aprili mwaka huu, kuwa ACT- Tanzania imeruhusiwa kubadili jina na kuwa ACT- Wazalendo.

Limbu na wenzake watatu, waliwasilisha mahakamani 30 Januari mwaka huu, maombi ya kuitaka mahakama kumzuia Samson Mwigamba, Prof. Kitila Mkumbo na mawakala wao, kutojihusisha na chama hicho.

Amewatuhumu kufanya mapinduzi ndani ya chama; kuteka chama; kubadilisha bendera, nembo na sasa jina la chama. Kesi hiyo imepewa Na. 1 ya mwaka 2015.

Anasema, “Msajili anajua kuwa kuna kesi iko mahakamani. Lakini yeye kwa maslahi yake binafsi, anaingilia uhuru wa mahakama na kutoa maamuzi ya kuifuta ACT- Tanzania na kuingiza chama kingine cha ACT – Wazalendo.”

Anasema madai kuwa Zitto na genge lake wameteka chama chake – Alliance Change and Transparency (ACT-Tanzania) – kinadhihirishwa na taarifa ya Jaji Mutungi kwa vyombo vya habari inayotaka ACT – Tanzania, kurudisha cheti cha usajili walichopewa kwa jina hilo ili wapatiwe kingine chenye jina la ACT – Wazalendo.”

Limbu amesema “Jaji Mtungi akiwa pia ni mwanasheria aliyebobea anayafanya hayo akijua jambo lolote likiwa mahakamani halitakiwi kufanyiwa marekebisho.

“Tayari nimeiandikia barua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhusu wasiwasi wangu kwamba Jaji Mtungi anapewa rushwa ndio maana anafanya haya maamuzi kwa makusudi,” ameeleza Limbu.

Amesema, Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alieleza gazeti la MAWIO Jumatatu iliyopita kuwa chama kilicho kwenye orodha ya vyama hadi siku hiyo ni ACT – Tanzania.

Alipoulizwa na mwandishi wa gazeti hilo kuwa chama cha ACT – Wazalendo kipo na kinaongozwa na Zitto Kabwe alijibu “… sikijui chama hicho na hapa kwetu hakipo.”

Anasema, “Leo ACT ina kadi tatu tofauti. Je, kukubali na kuruhusu mabadiliko makubwa hayo ameshaingilia hatma ya kesi yetu. Anajua tutashidwa. Huu ni mpango mkakati ambao unafanywa na kila mtu sasa anajua. Nina mtaka Jaji Mutungi awambie watanzania kuna nini nyuma ya ACT – Wazalendo.”

Akizungumzia hatma ya chama chake, Limbu amesema “ACT – Tanzania bado ipo. Ofsi ya msajili impe Kabwe jukwaa. Asajili chama chake. Atuache na chama chetu. Huu ni uhaini.”


Chanzo:Jamii Forums

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...