Balozi
Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani akifungua mkutano
wa Mabalozi wa Heshima uliofanyika siku ya Ijumaa April 24, 2015
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mkutano huo ulizungumzia uwekezaji
na Utalii zikiwemo Changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo. Pia
katika mkutano huo uliokua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano
uliudhuria pia na Viongozi wa Taasisi za Diaspora wa Tanzania ambao
wanaguswa na kuiona nchi yao ikipiga hatua ya maendeleo katia sekta ya
uwekezaji na Utalii.
Abdul
Majid mwanaDiaspora Mtanzania anayeishi California nchini Marekani
akielezea huduma kwa wateja bado ipo kiwango cha chini nchini Tanzania
na jinsi gani ikiboreshwa inavyoweza kunua uchumi wa Tanzania.
Balozi wa Heshima Mhe. Kjell Berch akichangia na kuelezea majukumu ya Balozi wa heshima.
Rais
wa East Africa Diaspora Business Counsil Benedict Kazora ambaye pia ni
mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas akichanganua na kutoa
maelezo yanayoweza na kurahisiha maswala ya uwekezaji na kukosoa baadhi
ya makampuni yanavyowekeza Afrika kwa kujinufaisha yenyewe.
Karen
Hoffman Rais wa The Bradford Group kutoka New York akielezea sekta ya
Utalii na utangazaji wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Heshima Mhe.Cemil Teber kutoka New Mexico akichangia jambo.
Balozi
wa Heshima kutoka Ohio Mhe. Patrick Griswold akielezea sekta ya
uwekezaji na changamoto inazokutana nazo huku akitoa mfano wake mwenyewe
alipokua meneja mkuu wa General Tire miaka ya nyuma na tangia
alipoondoka kiwanda kikafa na sasa anatarajiwa kwenda tena Tanzania
kujaribu kukifufua upya kiwanda hicho.
Mkutano wa Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Heshima ukiendelea
Wakati wa chakula. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production
No comments:
Post a Comment