Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Siha ,Rashid Kitambulilo akimuongoza mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea eneo la
mwekezaji la Tanganyika Film and Safari ambako wafugaji jamii ya Masai
wanadaiwa kufanya uharibifu mkubwa.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na kamati ya ulinzi na
usalama wakitizama uharibifu uliofanywa na wafugaji jamii ya Masai.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitizama moja ya gari lililochomwa
moto na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji jamii ya Masai.
Askari Polisi walilazmika kuongeza ulinzi katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa ,Gama akiteta jambo na baadhi ya viongozi ambao ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.
Vikao vikiendelea eneo la mwekezaji.
Uharibifu mkubwa umefanyika ambapo nyumba 16 na magari tisa yameteketea moto.
Mwekezaji Peter Jones akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo lililomsababishia hasara kubwa.
Vikosi
vya askari Polisi kutoka Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro vililazimika
kupiga kambi kwa muda katika eneo hilo ili kuwadhibiti wafugaji hao.Na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment