Mtangazaji Salama Jabir na timu yake ndio wameongoza maswali kwa Young Dee.
Salama: “… Mara yako ya kwanza kuchora tatoo ulikuwa una miaka mingapi?…”
Young Dee : “…Actually
sikumbuki nilikuwa na miaka mingapi.. lakini ilikuwa ni kipindi ambacho
nilikuwa nimeanza kuandaa albam yangu inaitwa ‘The City of David’ ..
tatoo yangu ya kwanza imeandikwa ‘The City of David’.. hii ndiyo project
ambayo ninaifanya hadi sasa hivi kuanzia kwenye ‘dada anaolewa’..
‘tunapeta’ .. hadi sasa hivi nyimbo zangu zinazotoka ni project ambayo
nimeanza kuifanya muda mrefu.. nina kama miaka mitano kama sikosei kwa
hiyo miaka mitano iliyopita ndio nilichora tatoo yangu ya kwanza….”
Salama : “..Wewe
kwa jinsi ulivyo, unadhani utafanya muziki maisha yako yote, kwanza..
cha pili, kama ukiamua kuacha muziki na kufanya kitu kingine pengine
kufanya kazi Bank, ama UN, ama wherever.. hauhisi kwamba maamuzi yako
ambayo unayafanya sasa hivi yanaweza yakakugharimu kwa vitu vya baadaye…?”
Young Dee : “….
Sijawahi kufikiria kufanya kazi UN au Bank wala nini.. wala kuwa
mwanajeshi.. Sijawahi kufikiria hivyo, wala sitamani.. Wala sita-enjoy
na sitapenda na siwezi kufanya kitu ambacho sikipendi, lazima nifanye
kitu ambacho nakipenda.. hata ikibidi hakinilipi kabisa kama nakipenda,
naenjoy kukifanya then I will do it mpaka nitakapofariki….”
Muba : “…Ule
wimbo umetoa juzi unaitwa siyo mchoyo, nimesikia baadhi ya watu
wanaongea kwamba kweli kuna demu ambaye kabisa yupo, ni ukweli kwamba
ulimwandikia demu yoyote?…”
Young Dee : “…
Huyo demu ndiyo yupo.. yupo.. siyo mchoyo kweli.. mimi hata sikuutunga
sana yaani.. kwa sababu nimechoka kutunga siku hizi naongea kitu
ambacho nakiona…”
Muba : “..Wanasemaga
Young Dee anacopy sana style yani unasikiliza nyimbo za akina Lil Wayne
halafu unakuja kuchukua style katika mashairi ya mtu..?”
Young Dee : “…
Sijawahi kuchukua mashairi ya mtu.. kusikiliza ni kweli mimi nasikiliza
kwa sababu mimi muziki kwangu ni maisha yangu.. lazima nisikilize
muziki, usinichagulie nini cha kusikiliza…”Salama : “… Wewe ni kijana na umeanza kufanya kazi muda mrefu sana.. niambie shule yako ikoje…?”
Young Dee : “… Nimeishia O Level, mambo ya kifamilia nikashindwa kuendelea tena so ikabidi nitafute ugali kwa style nyingine.. ndiyo ikawa hivyo.. bado nafikiria kurudi shule lakini nitakapojua nini nakitaka shuleni.. nikishaweka akili yangu hivyo, then nitarudi shule…”
No comments:
Post a Comment