Pages

November 17, 2014

Stori 9 kubwa kwenye Magazeti ya leo Tanzania November 17 2014

news
MWANANCHI
Waziri wa Maji Professa Jumanne Maghembe  ameshangazwa na utitiri wa watu  wanaotaka kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu 2015 akisema nafasi hiyo ya juu nchini haifanani na mashindano ya urembo ambayo mtu yoyote anaweza kujaribu.


Alisema watu hao wanaojitokeza kugombea urais hawaelezi wanataka kulifanyia nini Taifa na akashauri wasioweza kueleza hoja  zao wasichaguliwe kushika nafasi hiyo.

“Urais unahitaji kuwa na sifa,dira na ajenda kwa Taifa,lazima mtu anayetaka kuwa rais  atueleze uchumi utakua vipi,naona watu wengi wametangaza nia,ni wazo zuri lakini wajitathmini kwanza”alisema Maghembe

Hata hivyo Maghembe alipuuza mjadala wa umri wa mgombea akisema kwamba hauna msingi na kwamba sifa kuu ya mgombea urais ni ajenda ya kuliletea Taifa maendeleo endelevu.

Alisema kwa kipindi hiki ni lazima mtu anayetaka urais awaeleze Watanzania  atawezaje kuivusha nchi katika uchumi wa kati,vnginevyo hafai kushika wadhifa huo.
MWANANCHI

Wagonjwa waliolazwa na kupatiwa matibabu katika kituo cha afya Lukole Wilayani Ngara,Mkoani Kagera wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kupata kipigo toka kwa Mganga wa kituo hicho ambaye aliwataka kushiriki kazi za usafi wa wodi na mazingira ya kituo hicho.

Wagonjwa hao walidai kuwa mganga wa kituo hicho  Fred Nyangosie waliwapiga wao na jamaa zao akiwataka wafanye usafi,huku wengine wakiwa ni wagonjwa wasiojiweza.

Walisema mganga huyo alifanya hivyo baada ya kuwakuta baadhi ya wagonjwa wakila chakula ndipo alipoanza kuwapiga akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wake na kuamua kuwaburuza hadi nje wagonjwa hao pamoja na ndugu zao waliokuja kuwaona.

Mmoja wa wagonjwa alisema yeye alifungiwa na Mganga huyo kwenye moja ya chumba maalum alichokiita ni maabusu ambayo hutumia kutunza vifaa vya hospitali.

Alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo Mganga huyo hakutaka kutoa chanzo cha kuwapiga wagonjwa hao na kusingizia kuwa ili aweze kuzungumza mpaka apate kibali kutoka kwa mwajiri wake.
MWANANCHI
Matumizi ya kubandika kope yametajwa kuwa na madhara makubwa kwa watumia na huenda yakasababisha upofu kwa siku za baadaye.

Mtaalam wa magonjwa ya ngozi John Urio alisema matumizi ya kope husababisha kunasa kwa uchafu na bakteria na takataka nyingine kuingia ndani ya macho kwa kunasa na kuondoa nje jicho.

Ubandikaji wa kope bandia pia unaweka mzio kwenye ngozi na hata macho ya mtumiaji husika  kwani madhara ya kope bandia si makubwa sana kama yale ya kutumia gundi katika ubandikaji huo.

“Gundi inayotumika kubandika kope hizo ina kemikali na ikiwa hazijabandikwa kwa uangalifu mkubwa kuna uwezekano mkubwa wa kemikali hizo kudhuru ngozi inayozunguka jicho na hata kwenye jicho lenyewe.

Pia matumizi hayo husababisha kupukutika kwa kope halisi na kuzifanya zisiwe katika ule ukuaji wake halisi na ubora wa awali.

NIPASHE
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe ameishukia Taasis ya Utafiti wa Twaweza kuwa haina uwezo wa kufanya tafiti za kisayansi.

Twaweza jumatano iliyopita ilitoa utafiti pamoja na mambo mengine ikionyesha baadhi ya majina ya wagombea urais wanavyokubalika na wannachi ikiwa uchaguzi ungefanyika September mwaka huu.

Katika orodha hiyo Membe alishika nafasi ya tano huku akitanguliwa na Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyeongoza kwa kupata asilimia13.

Membe alisema tafiti zimefanyika mapema kabla ya wakati kufika na bila kuzngatia  misingi kanuni na sera za kiutafiti na kwamba zinaweza kuichonganisha nchi nzima na dunia.

Alisema kila kipindi cha uchaguzi kote duniani unapokaribia kunakua na utafiti ambao hutoa muelekeo wa nchi hususani na uchaguzi huo,hivyo ni jambo jema.

NIPASHE
Matokeo ya ukaguzi uliofanywa na mdhibiti na mkaguzi mkuuu wa hesabu za Serikali kuhusiana na kuchotwa kwa bilioni306 kifisadi kwenye akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya benki kuu BoT umeiweka matatani ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali huku wakizitambua fedha hizo kuwa ni mali ya umma.

Ofisi ya AG inadaiwa kuingia matatani baada ya ripoti ya ukaguzi huo iliyovuja kubaini kwamba inahusika moja kwa moja kubaini katika kuisababishia Serikali hasara ya bilioni321 katika kashfa hiyo.

Pia Wizara ya Nishati na Madini,bodi ya Shirika la umeme Tanesco nazo zimetajwa na ripoti hiyo katika kuisababishia hasara Serikali.

Ripoti hiyo ipo kwenye vitabu vitatu ambapo kila kimoja kina kurasa zaidi ya 300 ambapo kitabu cha kwanza ni muhtasari wa ripoti,cha pili na tatu ni nyaraka za ushahidi.

NIPASHE 
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Nyandoto Wilayani Tarime Peter Mwikabwe mwenye miaka19  amekutwa mekufa kwa kujinyonga kwa kamba nyumbani kwao baada ya kuzuiwa kuuza ng’ombe wa baba yake .

Baba wa mwanafunzi huyo alisema mtoto wake alikwenda kwa ndugu yake na kumdanganya kuwa ametumwa achukue ngo’ombe amuuze kwa aji ya mahitaji ya shule lakini kabla hajapewa ngo’ombe hao walipiga simu nyumbani kwao kutaka kupata ukweli ndipo ikagundulika alidanganya na kunyimwa.

Baada ya kumkataza kutaka kuuza ngo’mbe kijana wake aliingia chumbani na walidhani amekwenda kulala lakini baada ya kimya cha muda mrefu waliingia chumbani kwake na kumkuta ananing’inia na kamba akiwa tayari amefariki.

Kamanda wa Polisi Tarime Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaasa vijana kuachana na tabia za kukimbilia maisha ya starehe ambayo hayana faida kwao.

NIPASHE
Wanandoa wawili wa jijini Mwanza wamefariki dunia baada ya kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao Mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Kagera alisema wanandoa hao walifariki baada ya mke kukatwa mapanga na mkewe katika ugomvi wa kifamilia wakati wa usiku.

Alisema mwanamke huyo wakati akishambuliwa aipiga .kelel za kuomba msaada lakini majirani walipooenda walikuta tayari amekata roho.

Kamanda huyo alisema baada ya majirani hao kugundua  mama huyo ameuawa na mumewe ambaye walimkuta eneo la tukio,walinyang’anya panga na kuanza kumcharanga mapanga mwanaume huyo hadi walipohakikisha amepoteza maisha hapo hapo.

MTANZANIA
Ukataji miti ovyo umeshika kasi maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Simanjiro hali inayoonyesha uwezekano wa eneo hilo kugeuka jangwa hivi karibuni .

Kasi hiyo ya uchomaji mkaa imekua tishio kwa maisha ya binadamu ,wanyama na mimea ambapowachomaji mkaa wamepiga kambi kwa miaka kadhaa wakikata miti  na kuchoma mkaa bila wasiwasi wowote.

Wachunguzi wa masuala ya jamii wamesemazaidi ya asilimia75 ya mkaa unaouzwa na kutumika jijini Arushaunatoka Wilayani humo.

Baadhiya wachoma mkaa wamesema hiyo ni miradi ya wakubwa ambayo huwahudumia wakati miti na kuchoma mkaa huo kwa malipo kidogo.

Ofisa Mtendaji wa kijiji Namalulu Thadeus alikiri kukithiri  kwa uchomaji wa mkaa katika maeneo hayo ingawa alikataa kuthibitisha ukataji miti huo kuhusishwa wakubwa kutoka Serikalini.

HABARILEO
Rais wa Uganda Yower Museven ameimwagia sifa Tanzania  kwa jitihada za kupambana na ujangili na kukuza utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Ukanda wetu ni wa Ikweta, lakini una maajabu kupita sehemu yoyote dunia kwani kuna barafu katika milima iliyopo kwenye ukanda huu wa joto ikiwemo Mlima Kilimanjaro,Kenya na Ruwenzori,mito mikubwa kama Nile na hata maziwa ukiachilia mbali wanyama””alisema.

Rais huyo alisema jitihada zinazofanywa kwa sasa ni za mazoea kwani baadhi ya watu walio katika nafasi za kutangaza utalii wanashindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi kiasi cha kukosesha mapato  nchi hizo.

Museveni alisema kuna haja ya kuongezaka kwa hoteli za kitalii katika ukanda huo ili watu wapate  ajira na watu wengi zaidi wapate malazi wawapo katika kutaii na hivyo kukuza maisha ya watu wanaoishi maeneo ya kitalii.

Alisifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na majangili wa meno ya tembo na kusema itasaidia kupunguza na hatimaye kuondokana kabisa na watu wnaaovamia na kuharibu urithi w nchi.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...