Pages

November 10, 2014

MGOMO WA MABASI WAKWAMISHA ABIRIA KATI YA ARUSHA -MOSHI LEO

Hali ilivyo katika Kituo cha Mabasi Arusha

Mmoja wa Abiria akiwa hajui la kufanya kutokana na mgomo wa Wamiliki wa Mabasi kati ya Arusha na Moshi leo

Wakazi wa jiji la Arusha leo wameingiwa na taharuki kutokana na abiria waliokua wasafiri kwa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Miji ya Arusha na Moshi mkoa wa Kilimanjaro kugoma ghafla na kuwaweka  katika mazingira ya sintofahamu.

Umoja wa Wamiliki wa wasafirishaji wa mabasi ya mikoa hiyo,Akiboa ulithibitisha kwa waandishi wa habari na kudai kuwa wamechukua hatua hiyo kutokana na faini nyingi wanazotozwa na askari wa usalama barabarani.

Abiria walionekana wakitangatanga wasijue la kufanya huku wapiga debe wa magari aina ya Noah yanaofanya safari zake hapa mkoani walionekana kusaka abiria.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas alionekana Kituo Kikuu cha mabasi akifatilia hali ya usalama na kisha kuondoka.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...