Mhariri wa Gazeti ya Citizen la hapa nchini,Bw. Richard Mbamba ambaye ni mmoja kati wanahabari waliowahi kushinda tuzo za "CNN MultiChoice African Journalist of the Year 2008" akisisitiza jambo wakati wa Semina ya simu moja kwa wanahabari wa Tanzania juu ya namna wanavyopaswa kufanya kazi zao,iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika,jijini Dar es Salaam.Semina hiyo imekuja ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika wa shughuli ya utoaji tuzo hizo za "CNN MultiChoice African Journalist of the Year 2014" itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
Sehemu ya wanahabari waliohudhulia Semina hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa toka kwa baadhi ya wanahabari nguli barani Afrika walioongoza semina hiyo.
Mhariri wa Gazeti ya Citizen la hapa nchini,Bw. Richard Mbamba akiendelea kutoa somo kwa wanahabari.
Mhariri wa Gazeti la City Press la nchini Afrika Kusini,Ferial Haffajee akizungumza wakati wa Semina ya simu moja kwa wanahabari wa Tanzania juu ya namna wanavyopaswa kufanya kazi zao,iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanahabari wa Tanzania wakiuliza maswali kwa wahariri hao.
No comments:
Post a Comment