Nakala ya Hati ya Kusafiria ya Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu ambapo inaonyesha ana miaka 25 sasa Aliyesema ana miaka 18, 23 tumueleweje?PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUMS.
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
..............................................
Hivi karibuni Katika Mitandao ya Kijamii kulizuka mada zinazoongelea Umri wa Miss Tanzania 2014 ambaye ameshinda taji hilo hivi karibuni katika Ukumbi wa Mlimani City.
Mara baada ya Mshindi huyo kutajwa yalizuka maneno ya chini chini ambayo awali katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook wadau wengi walianza kwa kuandika Kuwa "Na mimi nitajifunza Kichina ili Taji la Miss Tanzania Mwaka 2015 liwe langu" hawakuishia hapo baadhi ya wadau wengine pia waliandika Taji la Miss World litakuja Tanzania Kwa Sababu ya Kifaransa" wakaenda mbali zaid na kuamua kumuita Miss France ndipo hapo na mimi nikaanza kufuatilia kuna nini na nilipokuja kuuliza nikaambia etiiiii Wakati wa Maswali katika Shindano la Miss Tanzania lililofanyika Mwishoni mwa wiki iliyopita Mshiriki huyo ambae amebeba Taji hilo aliulizwa swali na kujibu Kwa Kifaransa...Ndipo nikagundua kuwa Kumbe Maneno yote yaliyokuwa yakisema na kuandikwa Kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook yalikuwa yanamuhusu yeye?????Mmmhhh Basi sawa......
Wakati hilo likiwa halijafutika masikioni na kwenye ubongo wa Watanzania si ndio likazuka Jingine sasa Unalijua ni lipi hilo........UMRI ndipo nikaanza kuangalia tena facebook kujua kuhusu hilo ndio nikakutana na Ujumbe Huu
Miss Tz 2014 ana miaka 18... Ana Masters!!!!
Piga hesabu:
Miaka 7-Primary
Miaka 4-O level
Miaka 2-A level
Mwaka 1-Masters
Miaka 3-1st Degree
Kwa hiyo alianza shule akiwa na mwaka 1...
Sasa mada hii nayo ikakua ikashika moto sas leo tena yakaibuka mapya ambapo nasikia kuwa Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania amesema Ana Miaka 23 ambapo alizaliwa mwaka 1991 hatujakaa vizuri Ikapatikana picha ya Paspoti yake ambayo inaonyesha kuwa ana miaka 25 sasa hii nayo Inataka Moyo....
........Basi Sawa Acha Movie iendeleeeee....Ni Hayo tu
No comments:
Post a Comment