Pages

October 7, 2014

Uzinduzi wa album John Lisu wafana sana Diamond jubilee hall

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira akionyesha album ya  ‘Uko Hapa’ yenye nyimbo 18 ya mwimbaji,  John Lisu wakati wa uzinduzi wa album hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, mwishoni wiki. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambaye ni mdhamini wa uzinduzi huo.
 John Lisu akiimba kwa hisia kali wakati wa uzinduzi wa Album yake ya 'Uko Hapa'
Mary Lisu (kushoto), akiimba sambamba na John Lisu wimbo mpya ujulikanao kwa jina la Mfalme ambao Albam yake iko jikoni wakati wa uzinduzi wa Album ya John Lisu ya 'Uko Hapa' uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Waimbaji wa John Lisu wakiwajibika jukwaani wakati wa uzinduzi wa Album ya 'Uko Hapa'.
Mary Lisu akiimba wimbo wa mpya ujulikanao kwa jina la Mfalme ambao Albam yake iko jikoni wakati wa uzinduzi wa Album ya John Lisu ya 'Uko Hapa' uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI  nguli wa muziki wa Injili Tanzania, John Lisu juzi alikonga nyoyo za mamia ya wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa albamu yake ya Uko Hapa yenye nyimbo 18, uliofanyika katika Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo uliofanyika mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Waziri Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu, Stephn Wassira, ulikuwa na mvuto mkubwa sio tu kutokana na umahiri wa mwimbaji huyo, pia maandalizi yaliyofanywa na wadhamini.

Lisu alipopanda jukwaani, alifanya kweli kwa kuimba nyimbo zaidi ya tano zilizopo katika albamu hiyo iliyozinduliwa.

Lisu aliyepanda jukwaani saa 12 jioni, alidhihirisha uwezo wake wa kushambulia jukwaa kwa kuimba hadi saa mbili bila kuonesha kuchoka.

Uzinduzi wa albamu hiyo uliofanywa na  Waziri Wasira, iliwekwa baraka baada ya kuzinduliwa na maaskofu watano  wa Makanisa tofauti.

Hao ni Askofu Lawrance Kametta (TAG-Jimbo la Mashariki), Askofu Deo Rubala (Word Alive Centre), Askofu Bruno Mwakibolwa, Mtume Peter Nyaga (RGC-Miracle Centre) na Machungaji Paul Safari (DPC).

Lisu alilitumia jukwaa hilo lililolipuka kwa shangwe za mashabiki alipoimba na mkewe, Nelly wimbo wake mpya wa Mfalme ambao unatarajia kuwemo katika albamu yake mpya ambayo ipo katika maandalizi.

Aidha, Lisu kabla ya kuimba na mke wake (Nelly), alitumia jukwaa hilo kuwatambulisha watoto wake mapacha na kuwabariki ambako pia alitoa ushuhuda baadaye watakuwa wachungaji.

Pia, jukwaani aliimba mojawapo ya nyimbo zake na muimbaji kutoka Kenya, Timoth Kaberia.
Aidha, Lisu alitumia fursa hito kutoa shukrani kwa waliofanikisha safari yake ya muziki huo. 

DVD hizo zilizozinduliwa ambazo idadi yake ni 18 zimegawanyika sehemu mbili ni pamoja na Wakusifiwa, Wastahili sifa, uko juu, Inuka, Uko Hapa, Nijaze, Nitaongozwa, Wastahili Bwana, Roho Mtakatifu na Mtakatifu.

Nyingine ni Yu Hai Jehovah, Atikisa, Upendo Upendo, Mataifa Yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua Macho, Haleluya na Mungu Ibariki.

 Naye Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni wadhamini wa uzinduzi huo, Alex Msama, alishukuru mapendekezo ya mabadiliko yaliyopendekezwa katika Katiba mpya ambayo yanawatambua wasanii.


Alisema kutambulika huko kumetokana na mshikamano uliopo katika ya wasanii na serikali hivyo alitoa wito kwa wasanii kuongeza jitihada za ufanikishaji wa kazi zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...