Tasnia
ya Bongo Flava imepata pigo baada ya msanii wa kundi la Wanaume Family
anaefahamika kwa jina la YP kufariki jana usiku baada ya kuugua muda
mrefu ugonjwa wa kifua.
Meneja
wa kundi la Wanaume Family amethibisha kifo cha msanii huyo na kueleza
kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu.
“Tatizo alikuwa
anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi
akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda
zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake
baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa
na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.” Fella ameiambia Bongo5.
Kuhusu ratiba ya msiba huo, Fella amesema itafahamika leo majira ya saa saba mchana.
Mungu ailaze pema roho ya marehemu YP. Amen!
No comments:
Post a Comment