Rais wa wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA), Nasra Gathoni akizungumza wakati
wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika
(AHILA) unaoendelea katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Meza Kuu.
Naibu Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Grace Saguti akizungumza wakati wa mkutano huo.
Naibu
Waziri wa Viwanda Janeth Mbene ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya
akimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati
wa mkutano huo.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akifungua mkutano wa 14 wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA) .
Baadhi ya wanachama wakifuatilia mkutano huo.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akitoa mada.
Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi cheti mwanachama wa Chama cha
Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA), Monica Samwel kutoka Tanzania
wakati wa mkutano wa 14 wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa AHILA, Nasra Gathoni.
Makamu
wa
Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi cheti Naibu Mwakilishi Mkazi
wa WHO, Grace Saguti wakati wa Mkutano Mku wa 14 wa Chama cha
Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Kushoto ni Rais wa AHILA, Nasra Gathoni.
Mwanachama wa AHILA akipokea cheti kutoka kwa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Mwanachama wa AHILA Monica
Samwel kutoka Tanzania akipokea zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais Dk.
Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa 14 wa Chama cha Wanataaluma wa
Habari za Afya Afrika. Kushoto ni Rais wa AHILA, Nasra Gathoni.
Makamu wa Rais, Dk. Bilal akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa AHILA.
Waandaaji wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Makamu wa Rais.
Wanachama wa AHILA wakiwa katika picha ya pamoja.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Mkutano wa 14 wa AHILA.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiagana na Rais wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika, Nasra Gathoni.
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU
wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, amewataka wataalam wa afya kutumia
teknolojia ya mawasiliano katika kusambaza haraka taarifa za magonjwa
kwa wananchi ili kuzuia maambukizi au kutoa tiba mahsusi kwa wakati
muafaka pindi ugonjwa unapoibuka.
Dk.
Bilal alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua Mkutano
Mkuu wa 14 wa Muungano wa Wataalam wa Watoa Taarifa za afya Afrika
(AHILA), na kueleza kuwa kufanya hivyo kutasaidia usambazaji haraka wa
taarifa muhimu.
"Kupeana
taarifa za mara kwa mara za afya na ujuzi miongoni mwa wadau kama
wagonjwa, wahudumu wa afya, watoa huduma, watunga sera, watafiti na
mashirika ya fedha ni muhimu sana katika kuboresha huduma za afya
nchini. Kuimarisha usambazaji wa taarifa katika sekta hii kutaleta
matokeo chanya katika kukabiliana na magonjwa kama Malaria na Ukimwi
ambayo bado yanatusumbua sana," alisema.
Alisema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa taarifa za afya hasa maeneo ya
vijijini na kwamba Tehama itarahisisha kusambaza taarifa hizo ikiwamo
namna wananchi wanaweza kujikinga na magonjwa.
Rais wa Ahila, Nasra Gathoni, alisema katika mkutano huo, watajadiliana
kwa kina namna watakavyotumia fursa ya ukuaji wa Tehama katika
kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya afya.
Alisema kwa kutumia Tehama taarifa za afya zitawafikia wananchi wengi
kwa wakati mmoja na pia wataalamu wa sekta hiyo wanaweza kubadilishana
ujuzi kwa urahisi.
Naye Naibu Waziri wa Afya, Janeth Mbene, alisema kwa kutambua changamoto
zinazoikabili sekta ya serikali imeanzisha idara ya kukusanya taarifa
mbalimbali za magonjwa na kuzisambaza.
Aliwashauri pia watafiti kutumia Tehama kusambaza taarifa zao kwa wadau hasa wananchi wa maeneo ya vijijini.
No comments:
Post a Comment