LUNDENGA AZUNGUMZIA SAKATA LA UMRI WA MISS TANZANIA 2014
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo
ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji
hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga
alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo
alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo .
Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa habari
"Katika
mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na
Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania
2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei
31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema
Lundenga mbele ya wanahabari hao.
Lundenga
aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki
yeyote mwenye mtoto kushiriki,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa
ana mtoto,hilo halina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao
ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto
alieomba kupiga nae.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo
ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha
kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wakazazi wake.
Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991i.Picha Kwa HIsani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment