Spika
wa Bunge kesho tarehe 26 Mei 2014 atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi
wa Semina ya 25 ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola ambayo
itafanyika hapa nchini kuanzia tarehe 25/05/2014 mpaka 31/05/2014.
Semina
hiyo ambayo ni mfululizo wa hatua za mafunzo na kubadilishana uzoefu
kwa Wabunge wa nchi wanachama wa CPA itahudhuriwa na Wabunge zaidi ya 60
toka nchi 18 ambazo ni Australia, Ghana, Seychell es, Kenya Uganda na Nigeria. Nchi nyingine ni pamoja na Sri Lanka, Bangladesh, Uingereza, Namibia, Pakistan
(Khyber Panktunkwa), Kiribati , Trinidad & Tobago, Guyana, New
Zealand na Scotland. Wajumbe wengine watatoka nchi
za Zambia, Malaysia, Swazila nd, Tasmania, Cook Island, Rajastan, New South Wales, Uttar Pradesh, Western Australia, Zanzibar, Tanzani a, Chandigara, Australia Capital Territory, South Australia, Cook Islands, na India.
Katika Semina hiyo, washiriki wa Semina hiyo watapata fursa ya kujadiliana mada mbalimbali ambazo ni pamoja na
(1) Nafasi ya CPA katika Jumuiya ya Madola;
(2) Bunge na Hali ya Siasa nchini Tanzania;
(3) Nafasi na Jukumu la Spika na Watumishi wa Bunge;
(4) Mbunge na Chama cha Siasa;
(5) Maadili ya Bunge, Uwazi na Uwajibikaji;
(6) Kamati za Bunge na Mfumo wa Kamati;
(7) Nafasi ya Bunge katika Mapambano dhidi ya UKIMWI;
(8) Bunge katika kutoa haki za binadamu;
(9) Bunge, Mbunge na Vyombo vya Habari;
(10) Mahusiano ya Bunge, Serikali na Wananchi; na
(11) Usimamiaji wa Fedha katika Mchakato wa Kidemokrasia.
Aidha Semina hiyo, inatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mashuhuri ambao ni pamoja na
(1) Mhe. Rebecca Kadaga, Mb
Spika wa Bunge la Uganda
(2) Mhe. Ronald Kiandee, Mb.
Naibu Spika wa Bunge la Malaysia,
(3) Mhe. Barry House
Spika wa Jimbo la Western Australia
(4) Mhe. Dr. Benjamin Bewa-Nyogo Kunbour
Mnadhimu Mkuu wa Serikali wa Ghana
(5) Dr. William Shija
Katibu Mkuu wa Chama cha CPA,
Miongoni mwa Watanzania watakaotoa mada katika Semina hiyo ni: -
(1) Dr. Philip Mpango
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango
(2) Dr. Ayoub Rioba
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(3) Ndg. Ludovick Utouh
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(4) Dr. Fatma Mrisho
Afisa Mtendaji Mkuu, TACAIDS
Bunge la Tanzania linawakilishwa na: -
(1) Mhe. Job, Ndugai, Mb, Naibu Spika,
(2) Mhe. Mussa Zungu, Mb;
(3) Mhe. Beatrice Shellukindo, Mb;
(4) Mhe. Prof. David Mwakyusa, Mb;
(5) Mhe. Zahra Hamad, Mb;
(6) Mhe. Ummy Mwalimu, Mb;
(7) Mhe. Highness Kiwia, Mb;
(8) Mhe. Lediana Mng’ong’o, Mb;
(9) Mhe. Lucy Owenya, Mb;
(10) Mhe. Vita Kawawa, Mb;
(11) Mhe. Zaynab Vulu, Mb;
(12) Mhe. Khalifa Khalifa.
Imetolewa na:
Jossey Mwakasyuka,
Mwenyekiti,
Sekretarieti ya Maandalizi ya Semina ya 25 ya CPA,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment