Pages

May 3, 2014

KATIBU MKUU WA CCM AWASILI KISIWANI PEMBA MCHANA HUU,KUFANYA MKUTANO WA HADHARA GOMBANI YA KALE JIONI YA LEO


 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba,Mchana wa leo tayari kwa Mkutano wa Hadhara wa CCM kwa Mikoa ya Miwili ya Pemba.wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Ndg. Mzee Mbelwa (kulia) akifatiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba,Abdallah Mshindo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai (katikati) akifurahia jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakati akimkaribisha Kisiwani Pemba leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba,mchana huu.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakisalimiana na baadhi ya wanaCCM wa Kisiwani Pemba waliofika uwanjani hapo kuwapokea.
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana ukitokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba kuelekea Ofisi Kuu ya CCM Pemba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...