Kipigo hicho katika mchezo wa pili wa Ryan Giggs tangu arithi mikoba ya David Moyes, kinaipa ahueni Sunderland na kuipeusha kwenye balaa la kushuka daraja.
Lilikuwa ni bao pekee la Sebastian Larsson dakika ya 30 ambalo limeirejesha Man United katika zama za vipigo chini ya Moyes, huo ukiwa ushindi wa kwanza wa Sunderland Uwanja wa Old Trafford tangu mwaka 1968.
Gundu pale pale: Wachezaji wa Manchester United wakisikitika baada ya kipigo
Asante mkongwe: Sebastian Larsson akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la ushindi Sunderland
Makocha wapya, gundu pale pale: Kocha Mkuu, Ryan Giggs na wasaidizi wake Nicky Butt na Paul Scholes
No comments:
Post a Comment