Jaji
mstaafu Mark
Bomani akiwa anazindua Rasmi albamu ya Mrisho Mpoto hii leo katika
maazimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani iliyofanyika
kitaifa katika ukumbi wa AICC jijini Arusha
Mrisho mpoto akitoa maelezo kidogo kuhusiana na Albamu yake aliyoizindua leo
Jaji mstaafu Mark
Bomani leo amezindua rasmi video
ya wimbo wa waandishi wa habari
ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu
pamoja na albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto
ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru wa vyombo
vya habari duniani.
Uhuru wangu uko wapi mwanahabari mie,kalamu yangu,sauti
yangu kamera yangu leo ndio kaburi langu mie
Huo ndio wimbo wa kundi la
Mrisho Mpoto Band ambalo ulikuwa ukiwaburudisha wanahabari katika
uzinduzi wa albamu Mrisho Mpoto Band,unaoelezea mambo mbalimbali wanayokumbana
nayo wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akighani mashairi ya wimbo huo katika uzinduzialisema poleni
sana misa Tanzania,TMF,MOAT,UTPC ,TCRA kama mtu ile timu ya watu watano
tuyioituma Ujerumani ,Norway,Sweden ipo wapi ripoti yake
Akiongea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo pamoja na wimbo
huo wa wanahabari msanii mrisho mpoto alisema kuwa yeye alifarijika sana pale
alivyofatwa na wanahabari na kumuomba
awatungie wimbo ambao unawahusu
wanahabari pamoja mambo ambayo yanawakabili.
Alisema kuwa wamekaa wakashauriana na timu yake na bendi
yake kuwa watu wasanii wengi wamekuwa
wakizindua albamu kwa kuweka viingilio
vikubwa kualika watu wengi lakini yeye binafsi ameamua kuzindua albamu hii katika siku hii ya waandishi wa habari kwa
kuwa wamemtoa mbali na anakitu cha kuwapa zaidi ya kuwapa zawadi hii ya kuzindua albamu yake mbele yao.
Alibainisha kuwa
mbali nakuzindua albamu hiyo pia kwa kuwa waandishi wamempa hadhi ya
kuwatungia wimbo pia anajitolea kuweka wimbo huu wa waandishi wa habari ndani ya
albamu yake ili kila mtanzania na mshabiki wake ambaye atanunua albamu
yake aukute wimbo ndani ya albamu yake.
“Hii albamu yangu itakuwa na nyimbo zangu zote ikiwa na
wimbo wa nikipata nauli adi nyimbo zake zote ambazo zinajulikana na kiukweli
najisikia kulia sana kupewa heshima hii nzito ya kuzindua albamu yangu na ata
jana nilivyokuwa nakuja uku nilikuwa na zunguma na mh bomani kuwa hii kwangu
itakuwa ni historia katika maisha
yake”alisema mpoto
Katika wakati wimbo huu ukiendelea wanahabari walionekana wakitoa machozi kwa
kuuzunishwa na tenzi zilizopo katika wimbo huu kwani msanii huu ameuimba
kiualisiazaidi.
No comments:
Post a Comment