Pages

May 3, 2014

2000 wafukiwa kwa udongo Afghanistan

Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.

Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.



Mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha mafuriko na madhara makubwa


Baadhi walipanda kwenye paa kusubiri msaada wa uokoaji

Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa wameanza kuwapa mikate na maji maelfu ya watu waliolala nje kwenye baridi kali wakiwa hawana makazi.



"Taarifa zinasema ardhi na matope yameendelea kuporomoka ambapo wengi ya waliokufa ni waokoaji ambao walikwenda kutoa msaada kwa wenzao."

Kuna taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine ya watu huenda wakawa wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima kuangukia kijiji k katika eneo la mashambani la mkoa wa Badakhshan unaopakana na mataifa ya Tajikistan,Uchina na pakistan.

Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.

Mwandishi wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...