Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro
(kushoto) akiwahutubia wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika
viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (wa pili kushoto) akitoa hotuba
yake kwa wanamahafali wa mafunzo ya jinsia katika chuo cha GTI leo. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Asseny Muro
pamoja na Mkuu wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP
Mtandao, Lilian Liundi (kulia) wakiongoza maandamano ya wanamahafali ya pili ya
Chuo cha GTI kuelekea ukumbuni kabla ya kuanza kwa hafla hiyo
Mkuu wa taaluma na mipango
wa GTI, Bi Doroth akitamka kuanza kwa sherehe za Mahafali ya Pili ya Chuo cha
Mafunzo ya Jinsia Tanzania (GTI) kwenye hafla ya mahafali hayo leo. Sehemu ya wanamahafali wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) wakiwa
kwenye sherehe za mahafali yao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Mabibo jijini Dar .
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro (kushoto) akimtunuku cheti cha jinsia mmoja
wa wahitimu wa mahafali ya pili ya chuo hicho leo katika viwanja vya TGNP Mabibo
jijini Dar es Salaam
Mmoja wa wanamahafali wa
Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya
kutunukiwa
Mmoja wa wanamahafali wa
Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akikabidhiwa cheti chake mara baada ya
kutunukiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro
.
Mmoja wa wanamahafali wa
Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) (kulia) akionesha cheti chake mara baada ya
kutunukiwa. Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi (kulia) akinong'ona
jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro kwenye
sherehe za mahafali ya pili ya Chuo cha GTI leo Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro, Mkuu
wa Chuo cha GTI, Zuki Mihyo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi na
meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wanamahafali baada ya kutunukiwa vyeti
vyao. Wanamahafali wakiimba wimbo wa taifa kabla
ya kuanza kwa sherehe za
mahafali yao leo.
Na Thehabari.com, Dar es
Salaam MAHAFALI ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) yamefanyika leo
jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho eneo la Mabibo.
Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 9 wamehitimu mafunzo ya njinsia ngazi ya
cheti. Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha
Mafunzo ya Jinsia, Asseny Muro alikipongeza chuo hicho kwa kuendelea kutoa
mafunzo ya jinsia nchini kwa ngazi mbalimbali jambo ambalo linawezesha wahitimu
kuwa na uwezo wa kuchambua na kutathmini sera na program anuai kwa mtazamo wa
kijinsia katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Aliutaka uongozi wa GTI
kwa kushirikiana na bodi kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo
hicho, ikiwemo changamoto za uhaba wa raslimali watu na fedha ili kuhakikisha
malengo ya chuo hicho ya kudahili wanafunzi wengi zaidi yanafikiwa na kuanza kwa
wakati.
"..Rai yangu niwaombe wewe
mkuu wa chuo kwa kushirikiana na bodi ya GTI mfanye kila liwezekanalo ili
kuwezesha mafunzo hayo kuanza mapema na hatimaye wanafunzi hawa na wengine
watakaopenda kuendelea na masomo yao hapa chuoni wafanye hivyo ili kutimiza
ndoto zao na matarajio yao," alisema Bi. Muro.
Aidha aliwapongeza
wahitimu kwa kufanikiwa kumaliza mafunzo yao na kuwataka wakaitumie elimu hiyo
kiufasaha kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kuwa wataalamu na mabalozi wazuri wa
masuala ya jinsia hapa nchini.
"...Nitumie fursa hii
kuwaomba mkawe wataalamu na mabalozi wazuri wa masuala ya jinsia hapa nchini na
kwa kufanya hivyo nchi itajivunia utaalamu wenu ambao kama utatumika vizuri
utaiwezesha jamii kuwa na mipango na utekelezaji wa shughuli za maendeleo...,"
alisisitiza.
Naye Mkuu wa Chuo cha GTI,
Zuki Mihyo akizungumza na wahitimu na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo
zimekuwa zikikwamisha utekelezaji wa mipango yake kikamilifu, hivyo kuiomba Bodi
ya chuo kusaidia kutatua changamoto hizo ili chuo kiendelee kufanya vizuri zaidi
katika mipango yake. Mahafali hayo ya Chuo cha GTI ambacho kinaendeshwa na
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) pia yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
TGNP Mtandao, Mary Rusimbi, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi,
wafanyakazi wa GTI na TGNP Mtandao pamoja na wageni waalik
No comments:
Post a Comment