HII NDIYO SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO NAMNA ILIVYOFANA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.
Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia
mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na
kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye
sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za
miaka 50 ya Muungano.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano
ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja
matofali kwa kutumia kichwa na mikono. Baadhi ya silaha za kijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo
mkubwa wa jeshi letu. Kikosi cha Wanamaji Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege
yaliofanyika kwenye Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano. Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa
Uhuru kwenye kilele cha miaka 50. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa
kikosi cha mwamvuli . Maandamano ya Pikipiki. Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano . Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu
waliorusha
No comments:
Post a Comment