Vijana
wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa
CCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia
matembezi kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja
vya sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Vijana wakionyesha uzalendo kwa kuonyesha skafu zao zenye jina la Tanzania
Ujumbe maridhawa ambao ndio gumzo la mjni kwa sasa.
Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda
mchache kabla ya kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana
mbali mbali .
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akienda kukabidhi bendera ya Taifa kwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete .
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
ameshikilia picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa
ameshikilia picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani
Karume baada ya kuzipokea kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya
Uzalendo.
No comments:
Post a Comment