Mume wa marehemu
Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera wakiwa kwenye harambee ya kuchangisha
fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa mpendwa wetu marehemu Zainab Buzohera
aliyefariki Jumamosi Jan 4, 2014 saa 2 usiku (8pm ET) WanaDMV walijumuika katika
harambee iliyofanyika Bladensburg, Maryland na kuchangisha $22,938 kiasi
kilichokuwa kinatakiwa ni $15,000 hii inamaanisha wanaDMV wanapoamua hufanya
kweli shukurani kwa wote walioshiriki harambee hii kwa njia moja au nyingine
lengo ni kufanikisha na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema tunashukuru kwa
kutuwezesha kufanikiwa harambee hii ya mpendwa wetu Zainab Buzohera. WanaDMV
tunawashukuru wenzetu wa New York waliofika kwenye harambee hii kuja kusaidia
kutimiza malengo.
Shangazi wa marehemu
Jasmine Bernett akiongea kwa niaba ya familia ya Buzohera huku akiwa amejawa na
uso wa huzuni aliwashukuru wote waliofika kwani lengo ni kusaidia kuchangia ili
mwili wa marehemu Zainab uweze kusafirishwa nyumbani Tanzania kwa mazishi na
matarajio ni kusafirisha siku ya Jumatano na kisomo kinatarajiwa kufanyika siku
ya Jumanne jioni mahali patatangazwa baadae.
Rais wa Jumuiya ya
Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akielezea utaratibu wa
harambee.
Umati wa Watanzania
waliokuja kwenye harambee.
Dada Tuma akielezea
utaratibu wa mnada utakavyokuwa.
washika mahesabu
wakijiweka sawa kabla ya harambee kuanza.
Watanzania waliofiika
kwenye harambee wakitoa michango yao kabla ya harambee
haijaanza/
Michango ikiendelea
kabla ya harambee.
Timu ya New York
ikitoa mchango wake.
Dada Tuma akiendesha
mnada.
Watanzania kutoka New
York katika picha ya pamoja.
Kutoka kushoto ni
Yunus, Bob Miano, Mmiliki wa Vizion One Abdallah Kitwara na Albert Mateso wakiwa
kwenye harambee.
No comments:
Post a Comment