Arusha
Wanakwaya sita, waumini wa kanisa katoliki parokia ya Mt. Kalory Rwanga, Usa River, wamelazwa katika Hospitali ya Mission na Tengeru,wilayani Arumeru baada ya kujeruhiwa vibaya kwa bomu linalodaiwa kurushwa na askari polisi muda mfupi baada ya kutoka kanisani kwenye mkesha wa mwaka mpya.
PICHA KULIA :
Tukio hilo limetokea juzi majira saa 6.30 mita 100 kutoka katika kanisa hilo, eneo la Kisangani, ambapo waumini mbalimbali walikuwa wakielekea majumbani kwao baada ya kumalizika kwa misa ya mkesha.
Mganga msaidizi katika hospitali ya misheni,iliyopo chini ya kanisa hilo, Fredrick Mathew amethibitisha kupokea majeruhi watano, huku wawili wakiwa kwenye hali mbaya na wengine wakiendelea vizuri.
Aliwataja maheruhi hao waliolazwa hospitalia ya mission kuwa ni bi,Theresia Lesitare (33),bw Philipo Ambrose (22),bw Alphonce Nyigo (19)bi Mary Merikiory Kwai (40) na bi Anna Mathew (19) wote wakazi wa Lake Tatu, Usariver.
Majeruhi mwingine ambaye hali yake sio nzuri, bi Annet Baltazar (16) amelazwa hospitali ya Tengeru.
PICHA KUSHOTO:
Alisema majeruhi hao waliumia sehemu za miguu na mapajani kwa kuchanwa chanwa na mlipuko wa bomu na baadhi ya vipande vya bomu vikitolewa kwenye miili yao na baadhi yao kushonwa kwa nyuzi kadhaa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi wa tukio hilo umeanza mara moja na taarifa ya uchunguzi ataitoa baada ya kukamilika.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, mmoja wa majeruhi hao Mary Marikiory, alisema baada ya kutoka kanisani kwenye misa ya mkesha ya mwaka mpya, yeye pamoja na wana kwaya wenzake, waliondoka kuelekeza makwao eneo la Lake Tatu.
Alisema wakiwa barabarani waliona gari la polisi likija kwa kasi na lilipowakaribia walisikia mlipuko na wakajikuta wakiwa wamelala kandoya barabara huku baadhi yao wakivunja damu miguuni na tumboni.
Alisema gari hilo la polisi aina ya Toyota Landcruiser halikusimama na lilipofika mbele walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya makundi ya watu mbalimbali waliokuwa wakionekana barabarani.
Alisema waliomba msaaada kwa paroko wa Kanisa hilo padri Patrick Njau, ambaye alitoa gari na kuwapeleka hospitali ya mission huku wengine wakipelekwa hospitali ya wilaya iliyopo Tengeru kwa matibabu zaidi.
Akizungumza huku akitokwa machozi baada ya kuwatembelea majeruhi, askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Josephat Lebulu, alisema anashangaa kutokea kwa tukio hilo na kusisitiza kuwa kanisa katoliki limechoka kuandamwa na matukio ya aina hiyo.
“Waumini wanakosa gani hadi watupiwe bomu, kwanini polisi wapo kimya hadi leo wasiseme kuna siri gani, na kwa nini kila siku ni Wakatoliki tu ndio wanaopigwa mabomu, tunataka haki itendeke, watu wametokea kanisani usiku, wamekosa nini, hii nchi ipoje, usalama upo wapi? Alihoji.
“Sisi tumekosa nini, kupigwa mabomu kila siku hapa Arusha? Tumeshuhudia Olasiti, tukashuhudia Soweto sasa ni hapa Usa,” alisema.
Alisema na hili kanisa hatutakubali hata kidogo, tunataka wahusika wawajibishwe na wale walioficha uovu huu wawajibishwe la sivyo viongozi walioficha uovu huu wawajibishwe, Mungu atasimama kwa ajili yetu,” alisema.
PICHA KULIA :
Askofu Josephat Lebulu wa jimbo kuu katoliki la Arusha akiangalia kwa uchungu baadhi ya vipande vya bomu baada ya kutolewa kwa baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hospital ya Misheni, USA RIVER jana.
Tukio hilo limetokea juzi majira saa 6.30 mita 100 kutoka katika kanisa hilo, eneo la Kisangani, ambapo waumini mbalimbali walikuwa wakielekea majumbani kwao baada ya kumalizika kwa misa ya mkesha.
Mganga msaidizi katika hospitali ya misheni,iliyopo chini ya kanisa hilo, Fredrick Mathew amethibitisha kupokea majeruhi watano, huku wawili wakiwa kwenye hali mbaya na wengine wakiendelea vizuri.
Aliwataja maheruhi hao waliolazwa hospitalia ya mission kuwa ni bi,Theresia Lesitare (33),bw Philipo Ambrose (22),bw Alphonce Nyigo (19)bi Mary Merikiory Kwai (40) na bi Anna Mathew (19) wote wakazi wa Lake Tatu, Usariver.
Majeruhi mwingine ambaye hali yake sio nzuri, bi Annet Baltazar (16) amelazwa hospitali ya Tengeru.
PICHA KUSHOTO:
Mwanakwaya ,bi Anna Methew akiwa amelazwa katika hospital ya misheni baada ya kujeruhiwa miguuni na mapajani na kushonwa nyuzi kadhaa.
Alisema majeruhi hao waliumia sehemu za miguu na mapajani kwa kuchanwa chanwa na mlipuko wa bomu na baadhi ya vipande vya bomu vikitolewa kwenye miili yao na baadhi yao kushonwa kwa nyuzi kadhaa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi wa tukio hilo umeanza mara moja na taarifa ya uchunguzi ataitoa baada ya kukamilika.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, mmoja wa majeruhi hao Mary Marikiory, alisema baada ya kutoka kanisani kwenye misa ya mkesha ya mwaka mpya, yeye pamoja na wana kwaya wenzake, waliondoka kuelekeza makwao eneo la Lake Tatu.
Alisema wakiwa barabarani waliona gari la polisi likija kwa kasi na lilipowakaribia walisikia mlipuko na wakajikuta wakiwa wamelala kandoya barabara huku baadhi yao wakivunja damu miguuni na tumboni.
Alisema gari hilo la polisi aina ya Toyota Landcruiser halikusimama na lilipofika mbele walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya makundi ya watu mbalimbali waliokuwa wakionekana barabarani.
Alisema waliomba msaaada kwa paroko wa Kanisa hilo padri Patrick Njau, ambaye alitoa gari na kuwapeleka hospitali ya mission huku wengine wakipelekwa hospitali ya wilaya iliyopo Tengeru kwa matibabu zaidi.
Akizungumza huku akitokwa machozi baada ya kuwatembelea majeruhi, askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Josephat Lebulu, alisema anashangaa kutokea kwa tukio hilo na kusisitiza kuwa kanisa katoliki limechoka kuandamwa na matukio ya aina hiyo.
“Waumini wanakosa gani hadi watupiwe bomu, kwanini polisi wapo kimya hadi leo wasiseme kuna siri gani, na kwa nini kila siku ni Wakatoliki tu ndio wanaopigwa mabomu, tunataka haki itendeke, watu wametokea kanisani usiku, wamekosa nini, hii nchi ipoje, usalama upo wapi? Alihoji.
“Sisi tumekosa nini, kupigwa mabomu kila siku hapa Arusha? Tumeshuhudia Olasiti, tukashuhudia Soweto sasa ni hapa Usa,” alisema.
Alisema na hili kanisa hatutakubali hata kidogo, tunataka wahusika wawajibishwe na wale walioficha uovu huu wawajibishwe la sivyo viongozi walioficha uovu huu wawajibishwe, Mungu atasimama kwa ajili yetu,” alisema.
No comments:
Post a Comment