Mamadou Ndala.
Kwa Msaada wa Mtandao
KANALI wa Jeshi la Serikali ya Kongo Mamadou Ndala, ambaye alikuwa mstari wa mbele katika mapambano makali na majeshi ya Umoja wa Mataifa yaliyowango’a waasi wa M23 ameuawa na waasi wa ADF katika mashambulizi pamoja na askari wengine watatu, kwa mujibu wa msemaji wa Serikali.
Kanali Ndala ameuawa kuamkia jana katika mapigano makali yaliyozuka hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mamadou Ndala , ambaye alisaidia kupata ushindi wa majeshi ya serikali dhidi ya M23 kikundi cha waasi mwezi Novemba mwaka jana, alikufa kutokana na majeraha ya risasi baada ya mashambulizi ya roketi juu ya gari lake karibu na kijiji cha Mazizi katika jimbo la Kivu Kaskazini.
“Kanali Mamadou Ndala ameuawa .
“Inavyoonekana ni ADF- Nalu [ kutoka Uganda ni waasi wenye nguvu ] na ndiyo waliyomuua kanali na walinzi wake watatu ,” Mende msemaji wa serikali aliliambia shirika la habari AFP.
“Hii ni kweli hasara kubwa kwa majeshi ya ulinzi na Jamhuri ya watu wa kongo, “
ADF- NALU imekuwa ikilaumiwa kwa mashambulizi na utekaji nyara karibu na mji wa Beni katika Kivu Kaskazini, ikiwa ni pamoja na vifo vya raia angalau 60 katika mashambulizi mawili ya mwezi uliopita.
Serikali ya DRC, pamoja Na askari 21,000 WA kulinda amani kutoka Umoja WA Mataifa, wanaendelea kujaribu kuwaangamiza makundi ya waasi Ni kazi ngumu katika mashariki ya nchi.
No comments:
Post a Comment