Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri(mwenye Kaunda suti) na viongozi wengine
wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani
cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya
Nzega.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri(kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nzega Bundala Kiwele (kushoto) wakibadilishana mawazo wakati
wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa
ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika
jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akitoa maoni wakati wa Kikao maalumu cha
Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu akitoa maoni yake wakati
wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa
ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika
jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali
wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia
taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali
kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkaguzi
Mkuu wa Nje wa Mkoani Tabora kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali (CAG) Mohamed Msangi alitoa taarifa ya ukaguzi wakati
wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa
ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika
jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Baadhi
ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakiwa katika Kikao
maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya
ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana
katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Jacob Mtalitinya akitoa
ufafanuzi wakati Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya
kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali
kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Mkuu
wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupulla akitoa ufafanuzi wakati Kikao
maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya
ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana
katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameuagiza Katibu Tawala Mkoa (RAS)
kuwachukuliwa hatua Wakuu wa Idara wote waliosababisha kuibuka kwa hoja
za ukaguzi wa Hesabu za serikali katika Halmashauri mkoani humo.
Aliyasema
hayo jana wilayani Nzega kwenye baraza maalumu la madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili na kujibu hoja za Mkaguzi wa
hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.
Mwanri
aliwataka RAS kuanza kuwachukulia hatua kwa kuwaondoa Wakuu wote wa
Idara ambao wamekwenda kinyume cha taratibu na hivyo kuzisababishia
Halmashauri zao kuwa na hoja.
Alisema
hoja nyingi ambazo zimeibuka zinasababishwa na wakati mwingine manunuzi
yaliyofanyika kukosa viambatanisho kama vile stakabadhi za malipo
yaliyofanyika na nyingine kutofuata taratibu za manunuzi jambo ambalo
linaloelekea katika matumizi mabaya ya fedha za umma.Mwanri
alisema Serikali haiwezi kumvumilia Mtendaji au Mkuu yoyote wa Idara
ambaye hana nidhafu katika matumizi ya fedha za umma na hivyo
kusababisha hasara ambayo inapelekea baadhi ya miradi kutokamilika.
Mkuu
huyo wa Mkoa alitoa Mwezi mmoja hoja zote zilizotolewa na Mdhibiti na
Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zinapata majibu ikiwa na kuwachukulia
hatua wale wote watakaobainika kusababishia Halmashauri ya Wilaya ya
Nzega hasara.Alimwagiza
Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha kwa wale ambao walisababisha hasara
Halmashauri hiyo kuwasiliana na Tamisemi hata kama wamehama warudishwe
waje wajibu hoja zinazowakabili.
Katika
hatua nyingine aliitaka Halmashauri hiyo kuja na utaratibu wa kulipa
madeni ikiwa ni pamoja na ile asilimia 10 kwa ajili ya vijana , wanawake
na walemavu.Alisema kuwa utaratibu huo ni lazima pia uonyesha jinsi pesa hizo zitakavyorejeshwa ili watu wengine waweze kukopa.
Naye
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu aliwataka watendaji
mbalimbali kuwa na uzalendo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya
kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha kila wanachokifanya kinazingatia
maslahi mapana ya umma.
Alisema moyo wa kizalendo ndio utasaidia kukwepa dosari mbalimbali zinazoibua hoja kutoka kwa Mkaguzi wa hesabu za serikali.Aidha
aliwataka Wadiwani na Watendaji kufanyakazi kwa ushirikiano katika
kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri kwa ajili ya maendeleo yao na
Taifa kwa ujumla.
Akiwasilisha
taarifa ya CAG inayohusu Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkaguzi Mkuu wa
Nje wa Mkoa wa Tabora Mohamed Msangi alisema katika mwaka wa fedha
2016/17 zilitolewa hoja 40 ambapo kati ya hizo 14 zimefungwa na hoja 26
zimesalia.
No comments:
Post a Comment