Pages

June 8, 2018

NACTE IMEFUTA USAJII KWA VYUO 20 , TISA VYASIMAMISHWA KUDAHILI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)limetengaza kufuta usajili wa vyuo 20 baada ya kubaini vimeshindwa kufuata tararibu zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo hivyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaim Katibu Mtendaji wa NACTE Dk.Adolf Rutayunga amesema uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia kifungu cha 20 cha kanuni za usajili wa vyuo vya ufundi 2001.

Amesema vyuo ambavyo vimefutiwa usajili tayari baraza limeshaviandikia barua vyuo husika kuvitaka vihakikishe kuwa wanafunzi waliko kwenye programu zinazotolewa na vyuo hivyo wanahamia kwenye vyuo vingine vilivyosajiliwa na baraza kutoa programu kama hizo.

Amevitaja vyuo vilivyofutiwa usajili ni Covenant College of Business Sdudies(Dar es Salaam), Mugerezi Spatial Technology College(Dar es Salaam),Techno Brain(Dar es Salaam), DACICO Institute of Business and Management(Sumbawanga) na Arusha Institute of Technology (Arusha).

Vyuo vingine ni Lisbon Business Collage(Dar es Salaam), PCTL Training Institute(Dar es Salaam), Royal College of Tanzania(Dar es Salam), Iringa RETCO Business College(Iringa) na Highlands Health Instutute(Njombe).

Vyuo vingine ni East African Institute of Entrepreneurship and Finacial Management(EAIEFM) (Arusha), Musoma Utali Collage (Shinyanga) na Mlimani School of Professional Studies(Dar es Salaam).

Pia kuna chuo cha Dinobb Institute of Science and Business Technology(Mbeya), Institute of Social Work(Mbeya), Regency School of Hygiene (Dar es Salaam), St.Peters College of Health Sciences(Dar es Salaam), Genesis Institute of Social Science(Dar es Salaam), Institute of Management and Information Technology(Dar es Salaam) na Boston City Campus of Business College(Dar es Salaam).

Pia Dk. Rutayunga amesema mbali ya kufuta usajili kwa vyuo hivyo wamesitisha program zisizoidhinishwa na baraza ambapo vyuo vitatu vimefutiwa programu.

Amefafanua kabla ya kuanza kuendesha mafunzo ya kozi yoyote ,chuo kinatakiwa kuhakikisha kuwa mtaala wa mafunzo hayo umepitishwa na baraza na idara itakayosimamia mafunzo hayo imekaguliwa na kuonekanwa kuendesha mafunzo hayo katika ngazi husika.

Amesema vyuo vitatu ambavyo ni Quality Development College (Masasi)kimefutiwa programu ya Medical Attendent, St.Glory Nursing School (Dar es salaam) wamefutiwa program ya Medical Attendant and Medical Labaratory Sciences na chuo cha Lake Victoria Disability Medical Training Centre(Mwanza) wamefutiwa program ya Nursing and Midwifery.

Wakati huohuo amesema jumla ya vyuo tisa vimesitishwa kudahili wanafunzi wapya kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019.Uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia kifungu cha 22(1) cha kanuni za usajili wa vyuo vya ufundi,2001.

Amesema wanafunzi waliopo waliodahiliwa kwenye vyuo hivyo wanaruhusiwa kuendelea na masomo kama kawaida mpaka watakapohitimu mafunzo yao.

Amevitaja vyuo ambavyo vimesimamishwa kudahili ni Montfort Business College (Dar es Salaam), Institute for Environment and Development Sustainability(Dar es Salaam) na Songea Clinical Assintant Training Centre(Songea).

Pia chuo cha Institute of Continuing and Professional Studies(Zanzibar),Tanzania Institute for Trade and Investment(Dar es Salaam), Institute of Research and Innovation Zanzibar(Zanzibar), Silva Business and Management(Dar es Salaam), Mbeya Polytechnic College(Tukuyu Campus) na Earth Science Institute of Shinyanga(Shinyanga).
1
  Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Adolf Lutayunga akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya NACTE Mwenge jijini Dar es salaam wakati akitangaza kufuta vyuo 20 vya ufundi ambavyo havijakidhi viwango na taratibu za usajiri uendeshaji wa vyuo nchini vya ufundi nchini kutoka kulia ni Dk. Marcelina Aloyce Baitilwake na Dk. Gema Modu Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Vyuo
6
Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Adolf Lutayunga akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya NACTE Mwenge jijini Dar es salaam wakati akitangaza kufuta vyuo 20 vya ufundi ambavyo havijakidhi viwango na taratibu za usajiri uendeshaji wa vyuo nchini vya ufundi nchini kutoka kulia ni Dk. Marcelina Aloyce Baitilwake na Dk. Gema Modu Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Vyuo kulia ni Mr. Twaha A. Twaha Mkuu wa Kitengo cha Udahili NACTE.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...